mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Saturday, October 22, 2016

Uchunguzi baada ya Twitter na mitandao mengine kuvamiwa na wadukuzi


uvamizi wa mtandaoImage copyrightPA
Uchunguzi umeanzishwa baada ya uvamizi wa mitandao kadhaa dhidi ya kampuni ya Marekani ulioathiri huduma za baadhi ya mitandao hiyo.
Twitter, Spotify, Reddit, Soundcloud na mitandao mingine yameathirika katika uvamizi wa mitandao.
Kumekuwa na hofu kuhusu tishio dhidi ya usalama wa mitandao ya Marekani wakati uchaguzi mkuu ukikaribia baada ya wavamizi kufanikiwa kufikia barua pepe za chama cha Democratic na baadhi ya mashirika ya uchaguzi nchini.
Mitandao hiyo ni wateja wa kampuni iitwayo Dyn ambayo inaitumia kuwasaidia wateja kupata mitandao hiyo wakiyatafuta.
DynDNS imeathirika na uvamizi wa data katika kinachojulikana kama shambulio la (DDos) jambo linalofanya kuwa vigumu kwa wateja kuyapata mitandao hiyo wanapoyatafuta.
Haijulikani wazi ni nani anayehusika na uvamizi huo au ni kwanini Dyn imelengwa.
Katika taarifa kwenye mtandao wake, Dyn imesema uvamizi huo wa DDoS ulianza mapema Ijumaa Marekani na kuathiri kampuni zaidi mashariki mwa taifa hilo.
uvamizi wa mtandaoImage copyrightTHINKSTOCK
Athari ya awali ya uvamizi huo ulisababisha baadhi ya mitandao kutopatikana wakati watu wakiyatafuta au wakati mwingine agizo linalotumwa katika mtandao kuchukua muda mrefu kabla ya kupokewa.
Watu wengi waliokuwa wanatumia mitandao ya kijamii walieleza kuwa, Reddit, Twitter, Etsy, Github, Soundcloud, Spotify na mitandao mingine ilikuwa vigumu kuyafungua.
Mitandao pia kama Paypal, Pinterest na Tumblr pia yanaarifiwa kuathirika.
Katika ujumbe kwenye Twitter, na uliosambazwa pakubwa, Github ilisema "tukio la kimataifa" linaathiri Dyn na kufanya kuwa vigumu kuyapata mitandao yake.
Athari ya uvamizi huo ulidhihirika kwa saa kadhaa na kufikia mchana Ijumaa, Dyn ilisema huduma zake zimerudi kama kawaida.

No comments:

Post a Comment