MKurugenzi wa kampuni ya Advanced Security Company Limited, Juma Ndambile (wa pili kulia) akimtambulisha bondia Francis Cheka (wa kwanza kulia) mbele ya bondia Geard Ajetovic (wa kwanza kushoto) huku promota Jay Msangi (wa pili kushoto) akishuhudia.
Promota Jay Msangi (katikati) akiutambulisha mkanda kwa mabondia Francis Cheka (wa kwanza kulia) na Geard Ajetovic (kushoto)
Bondia Francis Cheka (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Geard Ajetovic mara baada ya kukutana mara ya kwanza.
Bondia nyota wa ngumi za kulipwa nchini, Francis “SMG” Cheka amesema kuwa Mserbia anayeishi Uingereza, Geard Ajetovic atampa kipigo ambacho hata kisahau katika maisha yake katika pambano lao lililopangwa kufanyika Jumamosi, kwenye viwanja vya Leaders Club
Cheka alisema hayo walipokutana kwa mara ya kwanza katika mkutano na waandishi wa habari iliofanyika kwenye ukumbi wa Sinema wa Mlimani City jijini.
Alisema kuwa Ajetovic amekosea kukubali kupambana nay eye katika ardhi ya Tanzania kwani mwaka 2008 alishindwa kwa pointi kutokana na maamuzi ya majaji ambao walimpendelea.
“Nimejiandaa vilivyo kwa ajili ya pambano hili,nilikuwa Zambia nilikfanya mazoezi ya wiki mbili, huyu jamaa ananiita mimi babu wakati wote tumezaliwa miaka ya 1980, atajuta nakuambia, amenizalilisha sana nami nitamjibu ukumbini,” alisema Cheka.
No comments:
Post a Comment