mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Thursday, February 25, 2016

TIMU YA TENISI YA TANZANIA YASHIKA NAMBA MBILI AFRIKA


TENNIS

Timu ya mchezo wa Tenisi kwa walemavu (wheelchair tennis) ya Tanzania imeshika namba mbili Afrika katika mashindao ya mchezo huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Nairobi.
Hayo yalisemwa na kocha wa timu hiyo Bw. Riziki Salum leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na vyombo vya habari juu ya ushindi walioupata.
“Tumeshiriki zaidi ya mashindano mawili jijini Nairobi na tumekuwa washindi wa pili Afrika, timu zote mbili za wanawake na wanaume zimeingia fainali zikiwa na na jumla ya wachezaji saba wakiongozwa na nahodha Juma Mohamedy,” alisema Salum.
Salum aliongeza kwa kusema, chama cha Dunia cha mchezo huo kimeahidi kuwapa mualiko wa kushiriki mashindano ya Dunia yatakoyofanyika Japan mwaka huu kulingana na ratiba itakayopangwa.
Aidha, Bw.Salum alimshukuru mfadhili Bi. Latya Nassoro ambaye ameiwezesha timu hiyo kwenda kushiriki mashindano hayo kwa kuwalipia nauli ya kwenda na kurudi pamoja na malazi na chakula.
Kwa upande wake Bi. Latya Nassoro aliwahimiza na kuwaomba watu binafsi na makampuni kujitokeza kufadhili timu za Tenisi ili mchezo huo ufike mbali nchini na kupata ushindi ambao utarejesha makombe nyumbani na kuiletea nchi sifa na kuitangaza miongoni mwa mataifa kupitia mchezo huo.
Timu hiyo ya Tenisi ilishiriki mashindano ya Dunia yaliyofanyika mwaka 2013 nchini Uturuki na kushinda kombe la timu bora zilizoshiriki katika mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment