Afisa ustawi wa jamii Bw. Shija Numbu |
Wazazi wamehaswa kuwalea watoto wao pindi wanapokuwa wadogo hadi wanapofikia umri wa miaka 18 na kuwapa huduma za msingi ambazo mtoto anazihitaji
Hayo yamesemwa na Afisa Ustawi wa Jamii Bw. Shija Numbu wakati akizungumza na mmiliki wa blog hii na kulezea kwa undani zaidi kuhusu majukumu ya mzazi kwa mtoto kwa mujibu wa sheria za haki za watoto ya mwaka 2009
Amesema kwamba sheria hii inawataka wazazi kuwapa watoto elimu,malezi mazuri bila kusahau afya bora na kuhakikisha mtoto anakuwa katika muonekano mzuri
Mbali na hayo pia amesema kwamba ni kosa la jinai kwa mzazi kumuozesha mtoto wa kike aliyechini ya umri wa miaka 18 kwani atasababisha mtoto huyo kukosa haki ya kupata elimu pia kusababisha kupata madhara kwa kubeba mimba za utotoni
“Mtoto akiolewa chini ya umri wa miaka 18 kawaida viungo vyake vya uzazi vinakuwa bado havijakaza hivyo akibeba mimba nirahisi sana kupata saratani ya kizazi “Alisema Bw. Shija
Hata hivyo amesema kuwa wazazi ndiyo ngazi ya kwanza katika kupinga ndoa za utotoni pindi wanapoona watoto wao wanakwenda ndivyo sivyo ili waweze kuwasaidia kutimiza ndoto zao
Vilevile Bw. Numbu amezungumzia suala zima la ukeketaji kwa watoto na kusema kuwa dhana hiyo bado inaendelea katika mkoa wa Arusha na kwa sasa wanatumia njia mbadala katika kutizimiza adha hiyo ya ukeketaji kwa watoto
“Kwa sasa wanawakeketa watoto wakiwa wachanga hivyo mtu si rahisi kujua kwa sababu wanaogopa kutumia njia ya zamani kwa kuwa watajulikana hivyo bado tunaendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuhakikisha tunatokomeza dhana hii katika jamii” Alisema Numbu
Amesema kuwa hawajawahi kupokea kesi ya ukeketaji kwa wanawake katika ofisi zao kwa sababu jamii inogopa kwa kuhofia kuchukuliwa hatua za kisheria lakini mwaka 2012 walipokea kesi moja ya ndoa za utotoni na hadi sasa hivi hakuna kesi yeyote waliyowahi kupokea kuhusana na ndoa za utotoni pamoja na ukeketaji
No comments:
Post a Comment