mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Saturday, February 27, 2016

MWANAUME AJIFANYA MWANAFUNZI MIAKA 4 MAREKANI



Artur SamarinImage copyright
Image caption
Mwanamume mmoja kutoka Ukraine amekamatwa baada yake kujifanya mwanafunzi wa shule ya upili bila kugunduliwa kwa miaka minne Marekani.
Artur Samarin, 23, alijiunga na shule ya Harrisburg High, jimbo la Pennsylvania akitumia jina "Asher Potts" baada ya viza yake kumalizika muda wake 2012.
Amekuwa akijifanya kuwa mwanafunzi wa umri wa miaka 18 na alikuwa akichangia sana katika shughuli mbalimbali shuleni.
Alionekana Mei 2014 na mbunge Patty Kim, ambaye alipakia picha waliyopigwa pamoja kwenye Twitter.
Marcel McCaskill, ambaye amekuwa pamoja na Samarin katika mpango wa kujifunza hesabu na sayansi amesema ameshangazwa sana na kisa hicho.
"Kusema kweli, alikuwa mtu mzuri sana. Alikuwa mfano wa kuigwa, mtu ambaye ungelipenda mtoto wako awe kama yeye.”
Wakati wa kukamatwa kwake, alikuwa na leseni ya udereva aliyoichukua akitumia jina Potts pamoja na kadi ya malipo ya uzeeni aliyoichukua akitumia tarehe ya uongo ya kuzaliwa.
Polisi wanasema anakabiliwa na mashtaka ya wizi, wizi wa kitambulisho na kubadilisha rekodi za umma.
Afisa wa shule ya Harrisburg, Kirsten Keys, amesema idara yake inashirikiana na maafisa wa polisi wanaofanya uchunguzi.

No comments:

Post a Comment