mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Saturday, February 20, 2016

WAFANYABISHARA WA MATUNDA YALIYOKATWAKATWA


Bw. Enock Mwika akiwa katika eneo la biashara yake ya uuzaji wa matunda
 Mfanyabiashara wa matunda katika soko la kwa morombo jijini Arusha ameuomba uongozi wa jiji kuwatengea eneo maalumu kwa ajili ya kufanyia biashara hiyo.

Akizungumza na RFL NEWS blog bw. Enock Mwika amesema kuwa serikali haiwajali wao kama wafanyabiashara wa matunda hivyo ni vyema serikali ikawajali na kuwapatia eneo husika la biashara lisilokuwa na usumbufu.  

Baadhi ya matunda anayouza bw. Mwika
Bwana Enock ameeleza baadhi ya changamoto anazokutana nazo katika biashara hiyo ni pamoja na matunda kuharibika kutokana kukaa kwa muda mrefu.

Lakini pia ameeleza changamoto nyingine ni pale anapokwenda kuchukua mzigo na kukuta eneo la kuchukulia mzigo limebadilishwa hivyo analazimika kuingia gharama na kwenda eneo linalopatikana mzigo huo.

Naye bw. Felix Faustine amesema amefurahishwa na huduma hiyo kwani matunda yake ni mazuri na huduma yake kwa wateja inaridhisha.

Bw, Enock akimuhudumia mteja
Aidha bw. Mwika amesisitiza ombi lake kwa serikali ya jiji hilo kuwaangalia kwa jicho la tatu kwani hata wao hujipatia kipato kupitia biashara hiyo.

No comments:

Post a Comment