mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Saturday, February 20, 2016

MSAMA ATANGAZA VIINGILIO TAMASHA LA PASAKA, NI 5000

2
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishiwa habari wakati alipotangaza viingilia vya tamasha la Pasaka litakalofanyika katika mikoa ya Geita , Mwanza na Shinyanga, kushoto ni  Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha la Pasaka, Khamis Pembe.
………………………………………………………………………………………………………
KAMPUNI ya Msama Promotions imetangaza viingilio vya Tamasha la Pasaka mwaka huu kuwa ni shilingi 5000 kwa wakubwa na shilingi 2000 kwa watoto.
Akizungumza na Waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Alex Msama alisema viingilio hivyo vinaendana na tukio hilo ambalo mbali ya kumuimbia na kumtukuza Mungu pia lina dhamira ya kusaidia jamii yenye uhitaji maalum.
“Nawaomba wakazi wa mikoa Geita, Mwanza na Shinyanga kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha tamasha hilo,” alisema Msama.
Msama alisema kupitia viingilio vya tamasha hilo wanatarajia kutoa kipaumbele kwa wakazi wa mikoa itakayopitiwa na tamasha kwa baiskeli zaidi ya 100 za walemavu ambazo zitagawiwa mikoa mbalimbali.
Aidha Msama alisema waimbaji mbalimbali wamethibitisha  kushiriki tamasha hilo ambao wanaendelea na mazoezi ya kujiweka sawa.
Naye Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Khamis Pembe alisema wanaendelea na mikakati ya kuimarisha ulinzi kwa wakazi wa mikoa hiyo.

No comments:

Post a Comment