WAENDESHA VYOMBO VYA MOTO BARABARANI WAONYWA KUZINGATIA KUDUMISHA AMANI KWA KUFUATA SHERIA ZA BARABARANI
Dereva bodaboda wa mtaa wa kwa morombo jijini Arusha
Wamiliki na waendesha vyombo vya moto barabarani mkoani Arusha wameombwa kudumisha mahusiano mazuri na jeshi la polisi hasa kitengo cha usalama barabarani
Kauli hiyo imetolewa mbele ya waandishi wa habari na kamanda wa usalama barabarani mkoani Arusha Bwana Malsoni Mwakyoma nakusema ajali zimeendelea kupungua
.
Kamanda Mwakyoma amesema mahusiano mazuri kati ya jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani pamoja na madereva ndio imekuwa chachu ya kupunguza ajali za barabarani mkoani Arusha.
Mbali na hayo amesema sheria itaendelea kuchukua mkondo wake ipasavyo hasa kwakukabiliana na changamoto ya ongezeko la vyombo vya barabarani pamoja na ongezeko la watumiaji wa barabara.
VIlevile amewashukuru wachungaji na mashehe kwa kuendelea kuhubiri amani na kuwataka waumini kuzingatia alama na sheria za barabarani
Hata hivyo kamanda mwakyoma ameomba abiria kutoa taarifa mapema hasa wanapoona kuna uvunjifu wa sheria barabarani na kuwataka wananchi watii sheria za usalama barabarani
Nao wamiliki wa magari na bodaboda pamoja na madereva bila kusahau wananchi wamemshukuru kamanda Mwakyoma kumhakikishia kuwepo uhusiano mwema katika uwajibikaji.
No comments:
Post a Comment