UCHAFU ULIYO KITHIRI MAENEO MBALIMBALI KATIKA JIJI LA ARUSHA
uchafu katika katika kata ya sokoni one mtaa wa ololovono
Wananchi jijini Arusha wameulalamikia uongozi kuhusu suala zima la usafi hasa uwepo wa takataka katika mitaa yao.
Hayo yamesemwa na wananchi wa mtaa wa ololovono kata ya sokoni one Bw. Macha Molel na B.Elizabeth Ngowi walipokuwa wakizungumza na Mgonja blog leo hii na kutoa dukuduku zao
Wamesema mtaa wao una uchafu mwingi na ambao husababisha magonjwa ya mlipuko kama vile homa ya matumbo pamoja na kipindupindu.
Pia wananchi hao wameulalamikia uongozi kwa kutoshughulikia suala la usafi ipasavyo hasa mzabuni ambaye amepewa jukumumu hilo la kupeleka takataka katika eneo husika ambapo mara nyingi huchelewa wakati huo huo wananchi wanalipia shilingi 1500 kila mwezi kwa ajili ya usafi.
Naye mwenyekiti wa mtaa huo Yelome Wambura amekiri kuwa kuwepo kwa uchafu katika mtaa wake ambapo amesema mojaya sababu ni wananchi kutojal i suala la usafi na kusahau kuwa usafi ni af ya.
Pia amelalamikia wananchi kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu utunzaji wa mazingira ambapo baadhi yao hutupa takataka hasa mifuko ya malboro katika mitaro ya maji na kupelekea mitaro kuziba.
Vilevile amelalamikia suala zima la utoaji sabuni na kusema kuwa hutolewa kwa upendeleo ambapo hupelekea mzabuni kufanya kazi kwa matakwa yake yaani bila kufuata maelekezo husika.
Mwenyekiti huyo ameiasa serikali kutilia mkazo suala la usafi kwani usafi ndio nguzoya afya bora na kuitaka kusambaza vizimba kila mtaa kwaajili ya kuweka takataka.
No comments:
Post a Comment