Tanzania na Kenya zimezindua huduma ya kituo cha pamoja mpakani yaani One Border Post katika mpaka wa Holili (Tanzania)-Taveta (Kenya).
Wakizindua huduma hiyo na majengo ya kisasa Waziri wa Tanzania anayeshughulikia Nchi za nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki kikanda na ushirikiano wa kimataifa Balozi Agustin Mahiga na Phyillis Kandie ambaye ni Waziri wa Kazi na Afrika Mashariki upande wa Kenya wamesema huduma hii iliyozinduliwa ni msingi muhimu katika kuelekea kwenye Ushirikiano imara wa Afrika Mashariki.
Waziri Kandie amesema kuweka huduma za Mpaka wa Nchi mbili katika eneo moja kutakuza uchumi wa nchi zote mbili kwa haraka.
Balozi Mahiga wa Tanzania amesema hii ni moja ya hatua mojawapo za kuelekea katika matumizi ya sarafu moja.
"Mfano wa faida za mradi kama huu ni unaona itapunguza takribani 400 (barabara ikikamilika kutoka Mombasa kwenda Burundi) japo Gharama ni kufikia milioni 12 dola za kimarekani lakini Afrika Mashariki tutafaidika" Ameongeza Katibu Mkuu wa Mtangamano wa Afrika Mashariki Richard Sezibera aliyekuwepo kushuhudia ufunguzi huu.
Mradi huu ambao umechangiwa na Nchi wahisani pamoja na Kenya na Tanzania umesimamiwa na Trade Mark East Africa.
No comments:
Post a Comment