KADA WA CCM SALUM HAPI APONGEZA UTEUZI WA MAMA MIGIR
.
Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli amefanya uteuzi wa Mabalozi watatu kwa ajili ya kuwakilisha nchi yetu katika Balozi zetu nje ya nchi. Katika majina yaliyoteuliwa ni pamoja na Dr. Ramadhani Dau, Dr. Asha-rose Migiro na Mathias Chikawe. Sio kusudio langu kuwazungumzia mh. Chikawe na Dr. Dau kwa leo. Lakini hili la Dr. Asha-rose Migiro nimeshawishika kuchukua kalamu na kuandika. Msukumo mkubwa ulionifanya kuchukua kalamu yangu na kuandika umetokana na mazungumzo ya watu mbalimbali pamoja na makala tofauti zilizoandikwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari juu ya “Dr. Migiro amepanda au ameshuka”?
Wengine wakaenda mbali zaidi kujiuliza kama kwa nafasi alizowahi kushika anastahili kuteuliwa Balozi au la. Mbali na maswali haya ya ufahamu, wapo walioamua kuandika makala. Makala hiyo ambayo binafsi nachelea kuifananisha na hekaya za abunuwasi imejaa dhana zisizo na mifano na ushahidi wowote wa kidiplomasia zinazoelezea kukosoa uteuzi wa Rais Dr. John Pombe kwa Dr. Asha-rose Migiro.
Nimeamua kuandika ili kutoa elimu na kusahihisha hekaya hizo za abunuwasi. Katika medani za diplomasia duniani, Balozi ni muwakilishi wa Raisi katika nchi husika aliyopangiwa kuwakilisha. Pamoja na ukweli kwamba shughuli za Mabalozi zinaratibiwa na wizara ya mambo ya nje kiutendaji, lakini mamlaka ya uteuzi na hata utenguzi wa Balozi yako kwa Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Dr. Asha-rose Migiro amewahi kuwa Waziri wa wizara mbalimbali ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ikiwemo wizara ya mambo ya nje. Pia amewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa – UN kabla ya kumaliza muda wake na kurejea nchini ambako hata hivyo aliteuliwa tena kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Nafasi zote hizi alizowahi kushikilia Dr. Migiro hazizuii yeye kuteuliwa kuwa Balozi kama alivyofanya Mh. Rais Dr. Magufuli.
No comments:
Post a Comment