ELIMU YA UJASIRIAMALI VYUONI
Wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja na vyuo cha kati nchini wameshauriwa kujihusisha na masuala mbalimbali ikiwemo uchumi.
Hayo yamesemwa na mkurungezi wa mafunzo wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bwana Joseph Mayagila wakati akitoa semina ya mafunzo ya ujasiriamali katika ukumbi wa chuo hicho.
Bwana Mayagila amesema kuwa ni vyema kila mwanafunzi kujitafutia akiba ya kumwezesha pale atakapokwama katika mahitaji yake ya kila siku.
Amesema zipo njia mbalimbali za kujipatia mahitaji kwa kila mwanafunzi ukiachilia mbali ada kwani mwanafunzi anaweza kuanzisha biashara kidogokidogo mpaka pale itakapokuwa.
“Mwanafunzi anatakiwa kuwa mjasiriamali kwani anaweza kuuza vitu vidogovidogo kama pipi, kuwa mwanamuziki, kuuza nguo na maitaji mengine ambayo yanaitajika katika eneo la chuo”.
Aidha amesema ili kuweza kupata mtaji wa kuweza kuanzisha biashara ni vyema kujijengea mazoea ya kuwekeza kiasi kidogokidogo cha hela kila siku ili kuweza kufikia malengo.
Ameongeza kuwa kila mjasiriamali anatakiwa kusoma vitabu mbalimbali vya ujasiriamali ili kuweza kupata mbinu mbalimbali za kuendeleza biashara zao.
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vya kati wamesema elimu za ujasiriamali zimewapa mbinu mbalimbali za kuweza kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika biashara zao.
“Elimu au mafunzo haya yametufikisha mbali kiuchumi kwani tulikuwa tukianzisha biashara zinakufa lakini saizi hatupati shida hata kidogo kwani tumepata ufumbuzi zaidi”
Hata hivyo elimu hiyo imewawezesha baadhi ya wanafunzi kuwa na maisha mazuri kwani wamejiingiza katika masuala ya ujasiriamali na kuweza kujipatia mahitaji yao ya kila siku.
No comments:
Post a Comment