Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Nape Nnauye akiwa anakazia jambo kwa wafanyakazi wa kampuni ya magazeti ya serikali ya TSN kuhusu kuboresha kazi zao na kuandika habari zinazofichua maovu katika jamii na kusimamia haki bila kumuonea mtu.
Mhariri wa magazeti ya Daily News Bw.Charles Masele akimweleza jambo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Nape Nnauye(hayupo pichani) mapungufu mbalimbali ya kampuni ya TSN na kumwomba waziri uyo awasaidie kuiboresha kampuni hiyo.
Mwenyekiti wa RAAWU tawi la Tanzania Standard Newspaper(TSN) Bw.Oscar Mbuza akimweleza waziri Nape(kulia) changamoto mbalimbali ya wafanyakazi.
Sehemu ya wafanyakazi wa kampuni ya magazeti ya serikali(TSN) wakimskiliza Mhe. Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye(hayupo pichani).
Waziri Nape nnauye akipiga “Selfie” na mfanyakazi wa magazeti ya kampuni ya serikali ya TSN baada ya mkutano na wafanyakazi hao katika ofisi za kampuni hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya magazeti ya Serikali(TSN) wakifurahia picha ya pamoja na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Nape Nnauye.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye amewaasa wafanyakazi wa kampuni ya magazeti ya serikali ya Habari Leo,Daily News,SpotiLeo na Sunday News kuwa mstari wa mbele katika kufichua maovu katika jamii,kwani kwa kufanya ivyo watajijengea heshima katika jamii na kuongeza idadi ya watu kuwaletea kazi zao kwa ukaribu zaidi.
Waziri nape ameyasema hayo leo hii jijini Dar es Salaam katika ofisi za magazeti ya serikali(TSN) kwenye kikao na wafanyakazi wa kampuni hiyo.
“Acheni kumumunya maneno,msaidieni Rais katika kufichua maovu ya nchi yetu ila tu msimuonee mtu bali mtende haki na hasa mkosoe ili kujenga na kwa namna hiyo mtajijengea heshima kubwa katika jamii”.
Waziri nape pia aliitaka menejimenti ya kampuni iyo kubadilisha fikara zao kwa kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara ili kampuni iyo ijitegemee vyema katika mambo yake.
Pia aliitaka menejiment ya kampuni iyo kukaa chini na RAAWU ili wahakikishe wafanyakazi wanafata taratibu za kazi na kuwaasa kushughulikia vipaumbele vya wafanyakazi hao ambavyo ni vifaa vya kazi ambavyo kutokuwa navyo inapelekea kushuka kwa morali ya kazi na pia madai ya wafanyakazi yashughulikiwe ndani ya mwezi mmoja.
Nae Mwenyekiti wa RAAWU katika kampuni iyo Bw.Oscar Mbuza alimweleza waziri nape kuwa wanatambua haki na wajibu wa kila mfanyakazi na kwamba kumekuwa na ukiukwaji wa sheria,taratibu na kanuni kwa mtizamo wao na ivyo wanaomba yafanyiwe kazi ili kurudisha imani yao kwa viongozi wao.
Nao wafanyakazi mbalimbali wa kampuni iyo walieleza changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo kutokuwepo kwa bima ya afya,hawapandishwi cheo na kulipwa malimbikizo mbali mbali wanayoidai kampuni hiyo.
Mhe.Nape pia amehaidi kufanya vikao vya mara kwa mara na wafanyakazi wa kampuni iyo ili kuboresha mambo mbalimbali ya kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment