mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Saturday, February 20, 2016

KOCHA SUPER D AWASILISHA RAMBIRAMBI ZA WADAU KWA FAMILIA YA MAREHEMU MOHAMED CHIBUMBUI

 
Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta Rwakatare katikati akimkabidhi Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila ‘Super D’ mchango uliotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili ya rambirambi ya marehemu Mohamed Chibumbui kilichotokea  Mkoa wa Mtwara Wilaya ya Masasi kushoto ni katibu Mkuu wa shirikisho hilo Makole Mashaga Picha na SUPER D BOXING NEWS
……………………………………………………………………………………………………..
KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ amekabidhi fedha za rambirambi kwa wafiwa wa bondia Mohamed Chibumbui ambaye alikuwa anachezea timu ya taifa ya mchezo wa masumbwi nchini
Chibumbui  aliyefaliki Februari 10 alikuwa anasumbuliwa na ugojwa wa kisukari na alizikwa Februari 13 katika  kijiji cha Mihima kata ya Namupa Tarafa ya Mtama wilaya ya Lindi Mkoa wa Lindi
Bondia Mohamed Chibumbui alizaliwa Aprili 24 mwaka 1988 
Alianza kujifuisha mchezo wa masumbwi mwaka 2003 akiwa chini ya kocha  Juma Urungu ‘Mkebezi’ na timu ya Mavituzi baada ya hapo alihamia timu ya polisi kisha timu ya JKT na mwisho mapaka kifo kinamkuta alikuwa akichezea timu ya Magereza
Akizungumza wakati wa kupokea ubani huo uliotolewa na wadau mbalimbali wa masumbwi wakiongozwa na 
Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT  na Tanzania Boxing Fans  ‘TBF’ inayowakutanisha wadau mbalimbali  kwa njia ya mtandao wa Watsap Group mama wa marehemu Hadija Likamba ameshukuru kwa kukabidhiwa lambilambi hiyo kutoka kwa wadau wa mchezo wa ngumi nchini na kuzidi kuwaombea duwa ili mchezo wa ngumi usonge mbele
Nae baba wa marehemu Said Chibumbui amewashukuru wadau wote na kwamba wataendelea kushirikiana bega kwa bega ambapo watakaa kikao kwa ajili ya arobaini ya marehemu na kufikishiwa taarifa mke wa marehemu Bi. Latifa Andrea
Marehemu ameacha mjane  Ratifa Adrea na watoto wawili   Alhaj Mohamed Chibumbui (7) na Abubakari Mohamed Chibumbui (2) arobaini itafanyika nyumbani alipozaliwa marehemu Tandika Azimio Tambukareli eneo la Maputo 

No comments:

Post a Comment