mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Thursday, March 31, 2016

TRA Yakamata Magari Matano ya TFF Kutokana na Malimbikizo ya Kodi ya Bilioni 1.118


Mamlaka ya mapato nchini (TRA) imeibukia tena Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lakini safari hii haijapiga kufuli account za TFF badala yake imeondoka na magari matano yanayomilikiwa na shirikisho hilo kutokana na kulidai kiasi kikubwa cha kodi.

TRA imeamua kuchukua magari hayo ikitaka TFF kulipa deni la malimbikizo ya kodi mbalimbali wanayodaiwa ili warejeshewe magari yao.

Richard Kayombo ni afisa wa TRA amethibitisha kuyakamata magari hayo yanayomilikiwa na TFF lakini amefafanua sababu zilizopelekea kufanya hivyo.

“Ni kweli tumekamata magari matano ya TFF na hayo magari yamekamatwa kama sehemu ya mwendelezo wa kuweza kupata mapato yanayotokana na deni la kodi ambalo TFF hawajalipa.

“Mpaka sasa tunawadai billion 1.118 ambayo ni kodi mchanganyiko kuanzia mwaka 2010 hadi 2015. Ikumbukwe hapo nyuma tulikamata account zao kwasababu deni lilikuwa ni billion 1.6 na tukaweza kupunguza sehemu ya deni lakini bado halijaisha na ndiyo sababu ya kukamata hayo magari matano.”

Hii ni mara ya pili kwa TFF kupigiwa hodi na TRA ikilalamikiwa kulimbikiza madeni ya kodi, mara ya kwanza TRA ilizifunga account zote za TFF lakini safari hii wameamua kuyashikilia magari yao.

Kwa mujibu wa Kayombo, magari hayo yapo kwenye yard ya YONO likiwemo basi ambalo hutumiwa kuisafirisha timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

Breaking News: Wabunge Watatu Wafikishwa Mahakamani Kwa Tuhuma za Rushwa


Pichani kutoka kushoto ni Mbunge wa Mwibala,Mh.Kangi Lugola,Mbunge wa Mvomero Mh.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa Mh.Victor Mwambalaswa
**
Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wamefikishwa mahakama ya Kisutu leo kwa tuhuma za rushwa.

Wabunge hao ambao ni wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge wanatuhumiwa kushawishi na kupokea rushwa  ya shilingi Milioni 30 toka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo 

Wabunge hao wameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 5 kila mmoja na kesi itasikilizwa tena April 14

Nape Nhauye Atema Cheche..TFF Inao Uwezo wa Kumlipa Kocha Mkuu wa Taifa Boniface Mkwasa...


Serikali ya awamu ya tano kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye imesema kwamba Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF linapaswa kumlipa mshahara kocha wa timu ya taifa (Taifa Stars,) kwa sababu uwezo wa kubeba majukumu hayo wanayo.

Charles Boniface Mkwasa alichukua nafasi ya M-holland, Marti Nooij, Juni 21 mwaka uliopita na ilisemwa kwamba serikali itaendelea kuisaidia TFF kumlipa kocha wa timu ya Taifa na Mkwasa (kocha wa kwanza mzawa tangu 2006) angeendelea kulipwa mshahara kama ule ambao makocha wa kigeni walikuwa wakilipwa.

Mbrazil, Marcio Maximo aliifundisha Stars kwa miaka minne kati ya 2006 hadi mwaka 2010, Mdenmark, Jan Borge Poulsen alichukua nafasi hadi mwaka 2012 tinu hiyo ilipochukuliwa na Mdenmark mwingine Kim Poulsen ambaye naye aliisimamia hadi mapema mwaka 2014 alipopewa majukumu hayo Nooij.

Makocha wote hao walikuwa wakilipwa mishahara yao na serikali iliyopita ya awamu ya nne chini ya rais mstaafu, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

Licha ya TFF kusema kwamba Mkwasa ataendelea kulipwa kiasi cha Shililindi milioni 25 za kitanzania kama mshahara wake wa mwezi na serikali ya Kikwete kudai itaendelea kuwalipia, Mkwasa amelipwa mshahara huo mara moja tu (Mwezi Julai, 2015)

Kufikia mwezi huu katika mkataba wake imebainika kwamba kocha huyo anadai kiasi kisichopungua milioni 200 kama malimbikizo ya mishahara yake.

NI juzi tu rais wa serikali ya awamu ya tano, Mh. John Magufuli alisema kuwa serikali yake itapunguza kima cha juu cha mishahara na kufikia milioni 15 kama mshahara wa mfanyakazi, na kiwango cha chini alisema kitakuwa milioni 1.5 kwa maana hiyo mshahara wa Mkwasa (milioni 25 kwa mwezi) hautakiwi pia katika serikali yake.

Kitendo cha serikali ya awamu ya tano kusema kwamba, TFF inapaswa kumlipa mshahara kocha wa timu ya Taifa kinaweza kuonekana ni pigo kwa Mkwasa lakini kwa namna yoyote ile Shirikisho linapaswa kufanya hivyo kwa kuwa Stars ni timu yenye udhamini mkubwa, pia TFF wanaweza kutumia njia nyingie za kujiingizia kipato chao kupata pesa za kumlipa mshahara kocha wa Stars.

Kila mtu ameona kazi iliyofanywa na Mkwassa kuanzia mchezo wake wa kwanza dhidi ya Uganda katika harakati za kufuzu kwa fainali zilizopita za CHAN. Mkwassa amesema kwamba amekubali kufanya kazi yake bila tatizo licha ya kutolipwa mshahara kwa miezi 8.

Ndiyo kama alivyosema mwenyewe kwamba yeye ni ‘mzalendo’ ndiyo maana ameendelea kufanya kazi yake lakini umefika wakati wa TFF kuwajibika yenyewe tena kikamilifu katika malipo ya mishahara ya timu za Taifa.

Hakuna uzalendo wa kufanya kazi miezi nane mfululizo bila kulipwa mshahara na Mkwasa anaweza kuzungumza hivi kwa uoga tu ama kulinda kibarua chake lakini katika uhalisi ni kitendo ambacho hakifurahii. Naungana na Waziri aliyesema kwamba, TFF inapaswa kumlipa kocha wa timu ya Taifa kwa kuwa uwezo huo wanao.

Za Mwizi ni Arobaini..Wezi wa Nyaya za Kampuni ya TTCL Wakamatwa


WANANCHI  wa Mtaa  wa soko la sovya Wilayani Kasulu usiku wa kuamkia leo wamewakamata wezi waliokuwa wamekata nyaya za mawasiliano za kampuni ya TTCL. 

Akiongea juu ya tukio hilo Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya simu TTCL nchi Dk Kamugisha Kazaura alisema kuwa tukio hilo limetokea katika eneo la soko la sovya majura ya saa kumi na moja alfajiri. Alisema kuwa wananchi  wanaoishi karibu na eneo lililokatwa nyaya hizo ndiyo waliowakamata vijana hao baada ya kufanya uhslifu huo. Mkurugenzi huyo alisema kuwa hasara waliyoipatia kampuni kwa kukata nyaya hizo inakadiliwa ni zaidi ya milioni 20.

"Hasara waliyoingizia serekali ni kubwa sana hizo nyaya walizokata zinagharimu milioni 20,lakini kuitengeneza upya line hiyo inaweza kugharimu zaidi ya hiyo fedha''alisema Kazaura

Alisema kutokana na wezi huo umepelekea baadhi ya ofisi za serekali kukosa mawasiliano ikiwemo ofisi ya polisi Wilaya,Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Bank na Takukuru. Naye Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano profesa Makame Mbawala alivitaka vyombo vya dola kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wezi hao wanaohujumu mawasiliano. 

"Hawa muwapeleke kwenye sheria hiki walichofanya ni kosa kwa sheria ya mwaka 2015 wanatakiwa kulipa faini isiyopungua milioni 50 au kifungo jela ili iwe fundisho kwa wengine"alisema profesa Mbawala

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya March 31, Ikiwemo ya Nchi Inavyotafunwa na Wajanja Kila Kona






Boss wa Clouds FM Ruge Akanusha Gerald Hando na PJ Kuacha Kazi...


MKURUGENZI wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba,  leo kupitia kipindi cha Power Breakfast‬ amekanusha uvumi wa watangazaji wa kituo hicho, Gerald Hando, Abel Onesmo na PJ,  kuacha kazi.
“Kwa nafasi yangu kama mkurugenzi,  taarifa nilizonazo ni kwamba tuna mikataba na wafanyakazi hao ambayo inaisha leo tarehe 31.  Sehemu kubwa ya wafanyakazi  wetu mikataba yao inaisha mwezi huu, hivyo  katika hali ya kawaida huwa tunatoa nafasi ya kumwambia anayetaka kuendelea na mkataba aandike barua au aseme,” alisisitiza Mutahaba.

Serikali ya Tanzania Kuingiza Nchini Ndege 2 za Kisasa Kutoka Canada Ndani ya Siku 60


Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano ya ushirikiano wa anga na Serikali ya Quwait. 

Makubaliano hayo yatawezesha mashirika ya ndege ya nchi zote mbili kufanya safari za moja kwa moja na kukuza sekta ya utalii.

Wakati hayo yakijiri, Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi imethibitisha kwamba imeagiza ndege za kisasa kutoka nchini Canada ambazo zinatarajiwa kuwasili nchini ndani ya siku 60 (miezi miwili ijayo).

Kwa kuanzia, awamu ya kwanza ya ndege hizo zitafanya safari za ndani bara na visiwani kabla ya kujitanua ndani na nje ya Afrika.

Shime watanzania, tusimame kidete na serikali yetu kuhakikisha kwamba tunaachana na unyonge wa kutumia ndege za mashirika ya nchi jirani. Hii ni fursa nzuri ya uwekezaji katika sekta ya chakula, nishati, vinywaji n.k.

Wafanyabiashara Wachina Kortini Kwa Kutorosha Noti za 500


Wafanyabiashara wawili raia wa China, Su Ning (39) na Feng Guang Quan (51) wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu ya kusafirisha Sh30 milioni kwenda nchini China, bila kibali cha Gavana wa Tanzania.

Washtakiwa hao wanadaiwa kusafirisha noti za shilingi miatanomiatano 60,000 kinyume na sheria ya ubadilishaji fedha na kwamba, kiwango hicho kilikuwa kimefungwa kwenye mabunda 40. Kila bunda moja lilikuwa na Sh500,000.

Hata hivyo, washtakiwa hao baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili, walikiri kutenda makosa hayo na Mahakama iliwasomea maelezo ya awali ambayo pia walikiri maelezo hayo, ikiwamo begi lililokuwa na mabunda 40 ya noti yenye thamani ya Sh20 milioni.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha, Wakili wa Serikali, Shadrak Kimaro akisaidiana na Estazia William walidai katika shtaka la kwanza, washtakiwa walitenda kosa hilo kati ya Agosti 15 na Agosti 31, mwaka jana.

Ilidaiwa kuwa washtakiwa walikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), wakisafirisha noti 10,000 za shilingi miatanomiatano kwenda nchini China, zenye thamani ya Sh5 milioni bila kibali cha Gavana wa Tanzania.

Hata hivyo, Hakimu Mkeha aliomba apewe muda ili aweze kujiridhisha kupita maelezo na vielelezo vilivyotolewa kabla ya kutoa uamuzi, kesi hiyo inaendelea leo.

“Kesi hii nimeiona ina vitu vingi kabla ya kufanya uamuzi naomba nipewe muda kupitia vielelezo ili kesho (leo) niweze kutoa uamuzi baada ya kujiridhisha ” alisema.

Mvua za masika zatabiriwa kuleta mafuriko

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes 
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua za masika katika ukanda wa Pwani, zinazotarajiwa kuanza wiki hii, zitakuwepo kwa vipindi vifupi na zitakuwa kubwa zitakazoweza kusababisha mafuriko. Aidha, kwa wakati huo hali ya joto kali itaendelea kuwepo nyakati za usiku huku ikipungua nyakati za mchana.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agness Kijazi alisema hayo jana wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na kueleza kuwa mvua za masika zimeanza kama ilivyotabiriwa huku ukanda wa Pwani zikianza wiki ya kwanza ya mwezi Aprili.
Dk Kijazi alisema ingawa maeneo hayo ikiwemo Jiji la Dar es Salaam, yanaonesha kuwepo mvua za wastani hadi chini ya wastani, lakini mabadiliko ya hali ya hewa yanafanya kuwepo vipindi vifupi vya mvua kubwa.
“Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo vipindi vifupi vya mvua kubwa wakati wa msimu huo wa masika na kuweza kusababisha hata mafuriko, ni vema wananchi kufuatilia utabiri wa hali ya hewa kwa vipindi vifupi,” alisema Dk Kijazi.
Alisema hali ya joto wakati huo wa mvua, inaonesha katika utabiri kupungua nyakati za mchana wenye kiwango cha juu cha joto huku usiku likiendelea kuwa kali kama ilivyo sasa licha ya kuwa kiwango chake ni cha chini.
Aidha, Dk Kijazi alisema kwa kutumia mtambo wa uchambuzi wanaotumia katika utabiri, utawezesha kutoa utabiri wa kimaeneo mara baada ya kuwa na vituo vingi vya hali ya hewa.
Alisema kwa Mkoa wa Dar es Salaam wana vituo viwili tu, lakini inatakiwa kuwa navyo 10 ili kutoa utabiri kwa maeneo na siyo kwa ujumla kwa kuchambua taarifa za kila kituo.
Akizungumzia mkutano huo wa Baraza la Wafanyakazi, alisema wanautumia kwa menejimenti na wafanyakazi kujadili maendeleo ya taaluma na kujadili bajeti yao kwa mwaka ujao ambayo wafanyakazi watashauri na kutoa vipaumbele.
Akizungumza katika mkutano huo, Mjumbe wa Bodi ya Mamlaka hiyo, James Ngeleja alitaka kutumia nafasi hiyo kujadili namna ya kuboresha utabiri wao kutoka usahihi wa zaidi ya asilimia 80 na kufikia asilimia nyingi zaidi.
Pia alitaka wafanyakazi kufanya kazi kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa kila mmoja kutenda kazi kwa nafasi yake ili kuongeza ufanisi wa mamlaka.


Mkoa wa Mwanza waongoza kuwa na watumishi hewa 334 ukifuatiwa na Mkoa wa Arusha kwa kuwa na watumishi hewa 270 ikiwa nchi nzima na watumishi hewa 2,702.

Hata hivyo Shinyanga na Songwe ni mikoa isiyo kuwa na watumishi hewa. Sababu kubwa iliyoiwezesha smShinyanga kutokua na watumishi ni matokei ya mikakati ya mkoa hu kupeleka majina ya watu wanaostahili kulipwa mishahara kila mwezi.

Akizungumza na Wakuu wa Mikoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene aliwataka wakuu wa mikoa wafanye kazi ikiwemo ubunifu wa miradi ya kuongeza mapato.

13 wadakwa na sare za JWTZ

Kamishna wa Polisi, Simon Sirro wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam akionesha bastola na sare za Jeshi ambazo wamezikamata katika msako unaoendelea jijini.
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa 13 kati yao wawili ni wanawake kwa tuhuma za kuwa na sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ). Aidha, limetoa onyo kwa watu wanaotumia vibaya majina ya viongozi mbalimbali.
Akizungumza na wanahabari jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema watuhumiwa hao walikamatwa Machi 23, mwaka huu maeneo ya Ulongoni ‘B’ katika Manispaa ya Ilala.
Kamanda Sirro alisema watuhumiwa hao walikamatwa baada ya askari kupata taarifa kutoka kwa wananchi kuwepo kwa kundi la wahalifu wakijiandaa kufanya uhalifu. Alisema askari walifanya ufuatiliaji na hatimaye kuwakamata watu hao wakiwa na vielelezo mbalimbali.
Miongoni mwa vitu walivyotuhumiwa kukamatwa navyo ni sare za jeshi hilo ambazo ni suruali tatu, mashati manne, fulana mbili, viatu vyeusi jozi mbili, kofia mbili zenye nembo ya JWTZ. Pia walikutwa na pikipiki moja aina ya Boxer yenye namba za usajili MC 444 AZL, mapanga mawili, sime mbili, visu na sururu mbili.
Akitoa onyo kwa wanaotumia vibaya majina ya viongozi, Kamanda Sirro alisema jeshi hilo linawatahadharisha watu mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara kuwa makini. Alisema watu hao hupiga simu na kutuma barua kutumia majina ya viongozi ili wajipatie fedha.
Alisema watakapokuwa na mashaka wanatakiwa kutoa taarifa katika jeshi hilo kama alivyofanya Mkurugenzi wa Kampuni ya Usangu Logistics baada ya kupokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa yeye ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Katika simu hiyo, alitakiwa kutoa punguzo la asilimia 25 za kodi na kwamba kila kampuni iliyolengwa na msamaha atatakiwa kulipa Sh milioni 25 kuboresha miundombinu.

JE Umeshawahi Kufikiria Mchezaji MBWANA SAMATTA Analipwa Mshahara Kiasi Gani Kwa Mwezi? Jibu Lipo Hapa


Klabu ya KRC Genk anayocheza nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta inatajwa kuwa miongoni mwa vilabu tajiri ndani ya Ligi Kuu Ubelgiji, ila kwa mujibu wa www.xpats.com, wachezaji wengi wao Ubelgiji hulipwa kati ya euro 25000 hadi 50000 kwa mwezi.

EURO elfu ishirini na tano ni zaidi ya milioni sitini za Kitanzania kwa sasa wakati Euro elfu 50 ni zaidi ya milioni mia moja ishirini za Kitanzania.

Hivyo Samatta Mshahara wake unaanzia uero 25000 na kuendelea..

RASMI..Gerald Hando, Paul James Waondoka Clouds FM


Watangazaji Gerald Hando na Paul James, wanadaiwa kuachana na Clouds FM, kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi.

Wawili hao wamekuwa watangazaji wa kipindi cha Power Breakfast cha kituo hicho kwa miaka mingi.

Gazeti la Mwananchi limedai kuwa watangazaji hao wamemaliza mkataba na kituo hicho na hakijapenda kuwaongezea.

Soma Hapa Barua ya Binti Aliyoandika Kabla ya Kujiua Kwa Kujinyonga Kwa Kutumia Kamba Huku Longido


Binti mmoja anayejulikana kwa jina la Jesca ambaye ni mfanyakazi wa Longido Mountain Lodge amekutwa amejinyonga katika hotel ya Longido Mountain Lodge na kuacha ujumbe kuwa kifo chake kisihusishwe na mtu yeyote 

Amesema amejinyonga kwa ridhaa yake mwenyewe.Katika ujumbe huo, ametaja majina ya watu anaowadai na kuagiza  walipe madeni yake kabla ya mwili wake kusafirishwa kwao pamoja na namba za Mama yake mzazi.

"Mimi Jesca Reinald Elisante Leo tarehe 29 , 03 , 2016 nimeamua kujinyonga kwa ridhaa yangu mwenyewe hakuna mtu yeyote anayehusika na kifo changu na hizi ni namba ya Mama  yangu,0672740439.

Ninao wadai
Mama Diana  33,000/=
John Memory card 4 GB
Boss Mshahara 60,000/=

wanao nidai
Zai 20,000/=alipwe na ninao wadai wahakikishe wanalipa kabla sijarudishwa kwetu.

NB:HAKUNA ANAYEHUSIKA NA KIFO CHANGU.
Ndugu zangu nawapenda sana
vitu vyangu vyote vipelekwe kwetu
Jau Kwenye Kuni."

Wananchi Waanza Kugombania Kiti Alichokikalia Rais Magufuli Kwenye Mgahawa Jijini Mwanza


Mgahawa aliotumia Rais John Magufuli kupata mlo wa mchana na msafara wake juzi kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza, umekuwa kivutio kwa wateja wengi wakinunua chakula na kutaka kukalia kiti na meza alivyotumia kiongozi huyo.

Meneja wa mghahawa huo wa Victoria, Elizabeth Maneno (pichani) alisema jana kwamba hali hiyo ilijitokeza mara baada ya Rais kuondoka hapo.

“Hata leo tumepokea wateja wengi kulinganisha na siku nyingine, baadhi yao wanaagiza chakula kwa sharti la kutaka kukikalia kiti na meza aliyotumia Rais Magufuli,” alisema Elizabeth.

Akizungumzia hali ilivyokuwa juzi kabla na wakati wa ugeni huo meneja huyo alisema: “Ilikuwa ni hofu na woga uliochanganyika na furaha kumwona Rais akiingia kwenye mgahawa wetu wa chai ya rangi ya Sh200 na ya maziwa Sh300.

“Mshtuko wetu uligeuka furaha baada ya kubaini kuwa oda ya sahani 28 za kubeba (takeaway), tulizoagizwa mapema asubuhi bila kuelezwa zinakoenda zilikuwa za ujumbe wa Rais,” alisema na kuongeza:

“Kabla Rais Magufuli hajaingia kwenye mgahawa wetu, alikuja mtu mmoja tusiyemfahamu na kuagiza sahani 28 za chakula kwa gharama ya Sh5,000 kila moja,”

Alisema baada ya kumtaarifu mteja wake kuwa chakula kiko tayari, alielekezwa kuandaa meza na viti kwa sababu wageni wake (wa mteja), sasa wameamua kula palepale mgahawani.

“Ghafla tulimwona Rais anaingia ndani ya mghahawa wetu; kwanza tulishikwa hofu, woga na kihoro tusijue tufanye nini hadi tulipogutushwa na aliyetoa oda kwa kutuagiza tugawe chakula alichoagiza,” alisema meneja huyo; “hapo ndipo tulipobaini kumbe chakula kile kilikuwa cha ugeni wa Rais.”

Pamoja na chai ya rangi na ya maziwa, mghahawa huo pia unauza vyakula vya aina mbalimbali kwa bei kati ya Sh1,500 hadi Sh5,000 kwa vyakula vya kubeba, huku soda ikiuzwa kwa Sh500 kwa chupa.

Nchi 10 kati ya 14 za Ulaya Zasitisha Misaada Tanzania


Tanzania tutegemee kuingia kwenye shida ya kiuchumi. Wale washirika wetu wa maendeleo yaan zile nchi za ulaya. Kwa kauli ya pamoja wamesitisha misaada katika nchi yetu. 

Tukumbuke misaada yao inaingia moja kwa moja kwenye bajet!! Wanaojua hatujitoshelezi. Kimaneno tunajitosheleza kwa 60% kivitendo hatuzid 40%.Ni zaid ya ile MCC. Maamuzi hayo yamekubaliwa na nchi 10 kati ya 14 za Umoja wa ulaya.

Swali kwa watawala hata hizo milijua hamtapewa mlijiandaa kujitegemea??
Maana ya MCC nilimsikia msemaji wa wizara ya fedha anasema waljua haztakuja hawakuziweka kwenye bajet.
Je na za washirika wa maendeleo hamkuziweka???

Wananchi mnatwambia tufunge mikanda suruali zetu zinavyotupwaya wakati nyie mnashindwa Hata kufunga vifungo vya makotI kwa vitambi.

Tuesday, March 29, 2016

Inabidi ujue Tanzania inao watu wenye pesa zao na wanayo malengo au mipango mikubwa zaidi ya kibiashara ambayo kama ikienda inavyotakiwa wanaweza kuifanya nchi hii kutajwa zaidi kuwa na matajiri miongoni mwa nchi zenye Mabilionea Afrika.

Kituo cha Television cha Marekani CNN kilimuhoji Mtanzania huyu na kikaweka kichwa cha habari ‘kutana na Bilionea mwenye umri mdogo Afrika‘ ni Mohammed Dewji ambaye ameajiri watu karibu elfu ishirini na nane kutokana na viwanda na biashara zake.

Mbunge huyu wa zamani wa Singida mjini amesema ‘nimekua nikitaka kununua Benki kwa miaka minne mitano iliyopita, sasa hivi nimeamua nataka kuanzisha Benki yangu kabisa japokuwa hii ishu ya Benki ya Barclays Afrika kuuzwa imekuja na nashawishika japo sijajua kama wanataka mnunuzi atakaeichukua Afrika nzima‘

‘Nimeshawishika kuinunua Barclays upande wa Afrika Mashariki na ninayo pesa tayari, sijajua wanaiuzaje lakini sina mpango wa kuichukua Barclays yote kwa Afrika, ningependa kuinunua upande wa Afrika Mashariki kwenye nchi za Kenya, Uganda, Tanzania yaani kwenye nchi nne au tano hivi’ – Mo
Dewji

March 24 2016 Mohammed Dewji aliandikwa na CNN kwamba anataka kuingia kwenye soko la ushindani Afrika na kushindana na Coca cola kupitia kinywaji chake cha Mo Cola na namnukuu akisema ‘tunashindana na Red Bull kupitia Mo Energy Drink’

Inabidi ujue Tanzania inao watu wenye pesa zao na wanayo malengo au mipango mikubwa zaidi ya kibiashara ambayo kama ikienda inavyotakiwa wanaweza kuifanya nchi hii kutajwa zaidi kuwa na matajiri miongoni mwa nchi zenye Mabilionea Afrika.

Kituo cha Television cha Marekani CNN kilimuhoji Mtanzania huyu na kikaweka kichwa cha habari ‘kutana na Bilionea mwenye umri mdogo Afrika‘ ni Mohammed Dewji ambaye ameajiri watu karibu elfu ishirini na nane kutokana na viwanda na biashara zake.

Mbunge huyu wa zamani wa Singida mjini amesema ‘nimekua nikitaka kununua Benki kwa miaka minne mitano iliyopita, sasa hivi nimeamua nataka kuanzisha Benki yangu kabisa japokuwa hii ishu ya Benki ya Barclays Afrika kuuzwa imekuja na nashawishika japo sijajua kama wanataka mnunuzi atakaeichukua Afrika nzima‘

‘Nimeshawishika kuinunua Barclays upande wa Afrika Mashariki na ninayo pesa tayari, sijajua wanaiuzaje lakini sina mpango wa kuichukua Barclays yote kwa Afrika, ningependa kuinunua upande wa Afrika Mashariki kwenye nchi za Kenya, Uganda, Tanzania yaani kwenye nchi nne au tano hivi’ – Mo
Dewji

March 24 2016 Mohammed Dewji aliandikwa na CNN kwamba anataka kuingia kwenye soko la ushindani Afrika na kushindana na Coca cola kupitia kinywaji chake cha Mo Cola na namnukuu akisema ‘tunashindana na Red Bull kupitia Mo Energy Drink’

Vigogo Wawili Maliasili Waliotoa Vibali vya Kusafirisha Tumbili Watiwa Mbaroni


Kikosi kazi maalumu cha kuchunguza makosa makubwa ya kihalifu kimewatia mbaroni vigogo wawili wa Wizara ya Maliasili na Utalii, wakihusishwa na utoaji wa kibali cha kusafirisha tumbili 61 kwenda nchini Albania.

Maofisa hao ni Mkurugenzi wa Idara ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Dk Charles Mulokozi na ofisa mfawidhi wa kituo cha uwindaji wa kitalii, utalii wa picha na Sites cha jijini Arusha, Nyangabo Musika.

Kikosi hicho kinaundwa na wachunguzi kutoka Polisi, Idara ya Uhamiaji, Usalama wa Taifa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kikosi cha kupambana na ujangili nchini na Takukuru.

Wakati Dk Mulokozi anakamatwa, tayari alikuwa amesimamishwa kazi kwa agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe kwa kutoa kibali wakati Serikali ilishazuia.

Vyanzo mbalimbali vimesema jana kuwa Dk Mulokozi alikamatwa mwishoni mwa wiki na jana alisafirishwa chini ya ulinzi kwenda kituo cha polisi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia).

“Hivi tunavyozungumza, Dk Mulokozi yuko njiani anapelekwa Kia chini ya ulinzi mkali wa polisi.Nyangabo yeye tayari yuko mikononi mwa vyombo vya ulinzi na usalama pale Kia,” kilidokeza chanzo chetu cha uhakika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alipoulizwa jana hakukanusha wala kukiri kuwa na taarifa za kukamatwa vigogo hao, lakini alisema atakuwa na mamlaka ya kuliongelea wakiingia mkoani kwake.

“Bado sijapewa hizo taarifa, lakini hata kama ningezijua nisingeweza kuzungumzia tukio la kukamatwa kwao lililofanyika mkoa mwingine. Nikikabidhiwa ndiyo naweza kusema chochote,” alisema Kamanda huyo. 

Hata hivyo, Waziri Maghembe alithibitisha kukamatwa kwa vigogo hao, akisema katika tukio hilo yeyote aliyetia mkono wake lazima akamatwe na kushitakiwa.

“Ni kweli Dk Mulokozi amekamatwa na siyo yeye tu kuna ofisa mwingine pale ofisi yetu ya Arusha naye tumemkamata. Hatuna mchezo katika suala hili,” alisisitiza.

Profesa Maghembe alitumia fursa hiyo kusisitiza kuwa raia wa Uholanzi waliokamatwa na polisi hawakuwa na vibali halali vya kufanya biashara ya kusafirisha wanyama hai kwenda nje ya nchi kama baadhi ya watu wanavyodai.

“Hawa Waholanzi walikuwa na tourist visa (waliingia kama watalii). Halafu Watanzania waelewe mtu hawezi kupata kibali cha kusafirisha mnyama hai kabla ya kumkamata, kuhesabiwa, akakaguliwa na kupata vibali stahiki,” alisisitiza.

Raia hao wa kigeni ambao ni ndugu wa familia moja, Artem Alik Vardanyian (52) ni mkurugenzi wa mgahawa huko Uholanzi na Eduard Alik Vardanyian (44), meneja wa hoteli huko huko Uholanzi.

Hata hivyo, vyanzo vingine vimedai  kuwa pamoja na kuwapo kwa vibali hivyo, lakini hapakuwapo na “release order” inayotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kama sheria inavyoelekeza.

Chanzo hicho kilidai wanyama hao walikuwa wasafirishwe kwa kutumia ndege ya mizigo ya kukodi ambayo ilitokea Afrika Kusini na ilikuwa iwapeleke wanyama hao Albania kupitia Nairobi nchini Kenya na Nigeria.

“Hao marubani wa hiyo ndege waliitwa pale Polisi (Kia), wakaandikisha maelezo yao kuwa walikuja kuchukua wanyama hao na wakaambiwa wao waondoke tu hakuna mnyama anaondoka,” alidokeza ofisa mmoja katika uwanja wa Kia.

Kutana na Bilionea Mtanzania Anaetaka Kuanzisha Benki yake… Anawazia Kuinunua BARCLAYS Tanzania!


Inabidi ujue Tanzania inao watu wenye pesa zao na wanayo malengo au mipango mikubwa zaidi ya kibiashara ambayo kama ikienda inavyotakiwa wanaweza kuifanya nchi hii kutajwa zaidi kuwa na matajiri miongoni mwa nchi zenye Mabilionea Afrika.

Kituo cha Television cha Marekani CNN kilimuhoji Mtanzania huyu na kikaweka kichwa cha habari ‘kutana na Bilionea mwenye umri mdogo Afrika‘ ni Mohammed Dewji ambaye ameajiri watu karibu elfu ishirini na nane kutokana na viwanda na biashara zake.

Mbunge huyu wa zamani wa Singida mjini amesema ‘nimekua nikitaka kununua Benki kwa miaka minne mitano iliyopita, sasa hivi nimeamua nataka kuanzisha Benki yangu kabisa japokuwa hii ishu ya Benki ya Barclays Afrika kuuzwa imekuja na nashawishika japo sijajua kama wanataka mnunuzi atakaeichukua Afrika nzima‘

‘Nimeshawishika kuinunua Barclays upande wa Afrika Mashariki na ninayo pesa tayari, sijajua wanaiuzaje lakini sina mpango wa kuichukua Barclays yote kwa Afrika, ningependa kuinunua upande wa Afrika Mashariki kwenye nchi za Kenya, Uganda, Tanzania yaani kwenye nchi nne au tano hivi’ – Mo
Dewji

March 24 2016 Mohammed Dewji aliandikwa na CNN kwamba anataka kuingia kwenye soko la ushindani Afrika na kushindana na Coca cola kupitia kinywaji chake cha Mo Cola na namnukuu akisema ‘tunashindana na Red Bull kupitia Mo Energy Drink’