Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Magufuli akihutubia Wakuu wa Mikoa wapya 26 na Watumishi wengine wa Serikali walioapishwa leo amesema; "Nimewateua ninyi (Wakuu wa Mikoa) muende mkawatumikie Wananchi na sio kwenda kufanya siasa.
"Ilinichukua muda sana kuteua kwa sababu nilitaka kujihakikishia kuwa ninateua watu makini.
"Mkienda Mikoani nataka mkatatue kero za Elimu, Ajira, Ujambazi na nyingine kwa kushirikiana na viongozi wengine na Mumtangulize Mungu naye atawasaidia.
"Kuna viongozi huko wananyanyasa wananchi, unakuta katibu tarafa, mtendaji wa kata ananyanyasa tu wananchi bila sababu.
"Ninyi mna mamlaka ya kumuweka mtu ndani hata masaa 48. Kawawekeni wengi ili kusudi wajue kwamba wananchi wanatakiwa kuheshimiwa." Amesema Rais
No comments:
Post a Comment