mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Monday, March 14, 2016

WABUNGE WAFUNDISHWA KUTUNGA SHERIA


pix 1 (8)Mkurugenzi Msaidizi wa Bunge Michael Chikokoto akiwasilisha mada mbele ya kamati ya Bunge ya  Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama pamoja na kamati ya Utawala na TAMISEMI zilipokutana kujadili mambo mbalimbali yahusuyo kamati hizo leo jijini Dar es Salaam.
PIX 2 (7)Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama Mhe. Balozi Adadi Rajabu  Mbunge wa Muheza akifatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa na maofisa wa Bunge mbele ya kamati ya Bunge ya  Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama pamoja na kamati ya Utawala na TAMISEMI zilipokutana kujadili mambo mbalimbali yahusuyo kamati hizo leo jijini Dar es Salaam.
PIX 3 B
PIX 3 APIX 3 (7)Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya  Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama pamoja na kamati ya Utawala na TAMISEMI wakifatiliamada zilizokuwa zikiwakilishwa katika semina iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaa
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania wamefundishwa jinsi ya kutunga sheria ikiwa ni moja kati ya kazi muhimu za Bunge katika semina za kamati mbalimblai za Bunge zinazoendelea kufanyika Jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yametolewa leo katika semina ya kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama pamoja na kamati ya Utawala na TAMISEMI zilipokutana kujadili mambo mbalimbali yahusuyo kamati hizo  ikiwa ni njia ya kuwakumbusha wabunge wajibu wao.
Akiwasilisha mada kuhusu kazi za Bunge na kamati zake kwa wabunge, Mkurugenzi Msaidizi wa Bunge Michael Chikokoto amesema dhumuni la semina hiyo ni kuwakumbusha wabunge wajibu wao ikiwemo suala la utungaji wa sheria za nchi.
“ Wabunge kazi yao sio kudhamini miradi tu ya maendeleo katika majimbo yao bali kuisaidia Serikali katika kuwasilisha mambo muhimu kwa kuwasilisha miswaada itakayopelekea kuwa sheria ambazo zitasaidia kuiendesha nchi” Alisema Chikokoto.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama Mhe. Balozi Adadi Rajabu  Mbunge wa Muheza amesema semina hizi ni muhimu kwa wabunge kwani zinawawezesha kuwapa uelewa wa kutosha katika masuala ya uuandaaji wa miswaada kuanzia mwanzo mpaka inapokuwa sheria.
” Semina hizi zinatupa mwanga hasa kwa wabunge wageni katika Bunge kujua ni kwa namna gani wanaweza kuandaa na kuwasilisha miswaada ikiwa ni pamoja na miswaada binafsi ama miswaada kupitia kamati mbalimbali za Bunge” Alisema Balozi Rajabu.
Aidha naye Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala na TAMISEMI Mhe. Jasson Rwekiza Mbunge Bukoba Vijijini amesema mbali na kuwawezesha wabunge kuelewa jinsi ya kutayarisha miswaada mpaka kuwa Sheria pia kamati hizi zina kazi ya kuangalia, kufatilia na kuhoji matumizi ya fedha za bajeti ya Serikali.
Kamati mbalimbali za Bunge zinakutana Jijini Dare s salaam ili kujadilia mambo mbalimbali yahusiyo kamati hizo kabla ya kuanza kwa mkutano wa tatu wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linalotarajiwa kuanza mwezi Aprili.

No comments:

Post a Comment