mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Sunday, March 13, 2016

Simba yachanja mbuga


nga wa Simba (kushoto) akiwania mpira na Salum Kimenya wa Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Simba ilishinda bao 1-0. (Na Mpigapicha Wetu).

SIMBA jana ilizidi kujichimbia kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifunga Tanzania Prisons ya Mbeya kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 54 na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, licha ya kuwa na mechi mbili zaidi ya Yanga iliyopo katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 51.
Yanga hawakushuka dimbani mwishoni mwa wiki baada ya kuwa na kibarua cha Ligi ya Mabingwa wa Afrika dhidi ya APR ya Rwanda, ambako waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 huku Azam FC nao waliibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya timu ya Afrika Kusini ya Bidvest Wits.
Bao hilo pekee katika mchezo huo liliwekwa kimiani katika dakika ya 87 na Awadhi Juma baada ya kupiga shuti kali akiwa nje ya 18 na kujaa wavuni. Simba walifanya shambulizi la nguvu langoni mwa Prisons katika dakika ya 14 wakati Hamisi Kiiza alipopata pasi nzuri ya Mohamed Hussein akiwa katika eneo la hatari lakini alishindwa kufunga.
Hassan Ramadhani nusura afunge katika dakika ya 17 lakini alipaisha mpira juu ya goli. Kiiza alishindwa tena kuifungia bao Simba baada ya kuwa katika nafasi nzuri ya kufunga lakini anababaika hadi mpira unawahiwa na kipa wa Prisons, Beno Kakolanya katika dakika ya 45.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa suluhu huku wenyeji Simba wakitawala zaidi kipindi hicho licha ya kushindwa kutumia nafasi nzuri walizopata za kufunga.
Dakika ya 49 Jeremiah Juma nusura aifungie Prisons bao alipopiga shuti lililopita pembeni ya lango. Ibrahim Ajib alipiga shuti kali katika dakika ya 52 lakini shuti lake liligonga mwamba na alikosa tena kufunga dakika mbili baadae lakini mpira wake ukaokolewa tena na kipa wa Prisons.
Kiiza alishindwa kuifungia bao katika dakika ya 66 baada ya kupata nafasi nzuri lakini shuti lake likagonga mwamba huku Prisons ikijibu dakika moja baadae na kutaka kufunga kupitia kwa Lambarti Sambiyanka.
Katika michezo mingine; Mgambo ilitoka sare ya bao 1-1 na Mwadui, huku Majimaji ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stand United na Kagera Sugar ikiilamba Coastal Union kwa bao 1-0

No comments:

Post a Comment