mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Monday, March 14, 2016

MRATIBU WA MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA HAPA NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI


01Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo ambaye pia ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Bw. Alvaro Rodriguez akimweleza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi nia ya Mashirika hayo ya kuisaidia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika masuala mbalimbali. Bw. Rodrequez alimtembelea Mhe. Kitwanga ofisini kwake leo. Kushoto ni Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) Bi. Gertrude Lyatuu.
02Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Charles Kitwanga akimwelezea Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) hapa nchini Bw. Alvaro Rodriguez (katikati) mipango ya Wizara yake ambayo inaweza kusaidiwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini. Bwana Rodriguez alimtembelea Mhe. Kitwanga ofisini kwake leo kuelezea nia ya Mashirika hayo ya kuisaidia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kushoto ni Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) Bi. Gertrude Lyatuu.
03Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo ambaye pia ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Bw. Alvaro Rodriguez akimwonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Charles Kitwanga mojawapo ya makabrasha ya Mashirika hayo yenye mipango ya maendeleo ya kuisaidia Tanzania. Bw. Rodriguez alimtembelea Mhe. Kitwanga ofisini kwake kuelezea nia ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kuisaidia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kutekeleza baadhi ya majukumu yake. Kushoto ni Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) Bi. Gertrude Lyatuu.

No comments:

Post a Comment