Habari kutoka visiwani Zanzibar zinaeleza kwamba, nyumba kadhaa ikiwemo ya Hamdani Omar Makame ambaye ni Kamishna wa Polisi Viswani Zanzibar zimelipuliwa kwa mabomu.
Habari hizo zinaeleza kwamba, Jeshi la Polisi linaendesha kamata kamata ya watu waliohusika kwenye tukio hilo ambapo mpaka sasa watu 31 wametiwa mbaroni.
Tukio hilo limezidisha hali ya wasiwasi visiwani humo ambapo ni siku 5 tu zimesalia kabla ya uchaguzi wa marudio kufanyika
No comments:
Post a Comment