Treni ya Mizigo ikiwa tayari kuanza safari katika eneo la Kidete Wilayani Kilosa, kufuatia kukamilika kwa ukarabati wa eneo hilo, uliodumu kwa takriban miezi miwili na hivyo kurudisha mawasiliano ya reli kati ya Mkoa wa Morogoro na Dodoma.
……………………………………………………………………………………
Huduma ya usafiri wa reli ya Kati iliyokuwa imesimama kwa takribani miezi miwili sasa imerejea kufuatia kukamilika kwa ukarabati wa reli hiyo katika eneo la kidete wilayani kilosa, mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hayo baada ya kukagua na kuridhika na ukarabati uliofanywa katika maeneo ya Magulu, Munisagara, Mzaganza na kidete Wilayani Kilosa.
“Hakikisheni mnailinda reli hii kwa manufaa yenu na ya Taifa, leo hii reli iko vizuri na treni ya kwanza kutoka Dar Es Salam kwenda bara itapita na kumaliza changamoto ya usafiri iliyokuwa inawakabili wananchi wanaotumiia reli hii”.Amesema Profesa Mbarawa.
Profesa Mbarawa amewataka wananchi wa maeneo ya Kilosa, Magulu, Munisagara, Mzaganza, Kidete, Godegodena Gulwe ambao maeneo yao yanakabiliwa na mafuriko ya mto Mkondoa kuacha Kilimo cha kuelekeza Maji kwenye reli bali washirikiane na Serikali kudhibiti maji hayo kwenda kwenye hifadhi ya reli.
AmesemaShirika la Reli Tanzania (TRL) linaendeleakuhakikisha kuwa treni inayopita kwenye reli ya Kati inapata mzigo mwingi wa kusafirisha kutoka bandarini za Tanga naDar Es Salaam kuelekea mikoa ya Mwanza, Kigoma na Mpanda, hivyo wafanyabiashara watumie fursa hiyo ili kupunguza mzigo unaosafirishwa kwa Nadia ya barabara.
Waziri Profesa Mbarawa ameteembelea bwawa la Kidete linaloelezwa kuwa chanzo cha mafuriko pindi linapojaa wakati wa mvua za Vuli na Masika katika mikoa ya Dodoma na Iringa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilosa John Henjewele amemhakikishia Waziri Profesa Mbarawa kuwa ofisi yake itafuatilia kwa karibu malalamiko ya wananchi wanaoishi karibu na reli ya Kati ili kuyapatia ufumbuzi na kuwataka wananchi hao kuitumia fursa ya kuwa karibu na reli kunufaika kiuchumi.
Takribani Shilingi millions 926 zimetumika katika ukarabati wa reli hiyo kufuatia uharibifu uliotokea mwezi Januari na kukata Mawasiliano ya reli Kati ya mikoa ya Dodoma na Morogoro na kusababisha Safari za treni kutoka bara kuishia Dodoma.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi,, Uchukuzi na Mawasiliano Serikalini.
No comments:
Post a Comment