mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Thursday, March 17, 2016

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI


MSANGIMTU MMOJA JINSIA YA KIUME AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI JIJINI MBEYA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KOSA LA KUHARIBU MIUNDOMBINU BONDE LA MTO MBALIZI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
` MTU MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA, JINSI YA KIUME MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 13 – 15 AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.979 ASP AINA YA TOYOTA RAV4 IKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE ARON ANYAMWILE [31] MKAZI WA UYOLE.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 16.03.2016 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO ENEO LA NSALAGA, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA USONGWE, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA, DEREVA AMEKAMATWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII AMBAO WAMEPOTELEWA NA NDUGU/JAMAA/RAFIKI KUFIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA UTAMBUZI.
KATIKA TUKIO LA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. TUWA JUMA [32] MKAZI WA SINDE AMBAYE ALIKUWA AKIENDESHA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.478 BPH AINA YA MITSUBISHI FUSO NA 2. GOD KAJANGE [25] MKAZI WA MBALIZI AMBAYE ALIKUWA AKIENDESHA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 328 ADX AINA YA MITSUBISHI FUSO KWA KOSA LA KUHARIBU MIUNDOMBINU YA RELI YA TAZARA KWA KUCHIMBA MCHANGA KUTOKA KATIKA ENEO LA NGUZO ZA RELI YA TAZARA KATIKA BONDE LA MTO MBALIZI.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 16.03.2016 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO ENEO LA MBALIZI, KATA YA SONGWE, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.
AIDHA KATIKA MSAKO HUO, MAGARI MAWILI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.617 ABU NA T. 609 ARL YOTE AINA YA MITSUBISHI FUSO AMBAYO MADEREVA WAKE HAWAKUWEZA KUPATIKANA YALIKAMATWA NA YAPO KITUO CHA POLISI MBALIZI.
SERIKALI ILISHAPIGA MARUFUKU SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MCHANGA KATIKA ENEO LA MTO MBALIZI KUTOKANA NA KUSABABISHA UHARIBIFU MKUBWA WA MAZINGIRA IKIWEMO MIUNDOMBINU YA RELI YA TAZARA HASA NGUZO ZINAZOSHIKILIA DARAJA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA WANAOISHI JIRANI NA BONDE LA MTO MBALIZI KUACHA UHARIBIFU WA MAZINGIRA IKIWA NI PAMOJA NA UCHIMBAJI MCHANGA NA KUWATAKA WAKAZI WA ENEO HILO KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO KWA KUKEMEA NA KUWAFICHUA WATU WANAOJIHUSISHA NA UCHIMBAJI MCHANGA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment