mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Monday, February 29, 2016

SPIKA WA BUNGE MH. JOB NDUGAI AKUTANA NA WABUNGE WA AFRIK MASHARIKI LEO


J1
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Job Ndugai akizungumza na wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) hawapo pichani kutoka Tanzania wakati walipomtembelea katika ofisi zake zilizopo jijini Dar es salaam na kumpa salaam maalum za kumpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwake na watanzania na kuwa Rais wa Tanzania awamu ya Tano ikiwa ni pamoja na kupongeza utendaji kazi wake kwa ujumla wake.(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
J2
Baadhi ya wabunge wa bunge la Afrika Mashariki waliomtembelea Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai kutoka kulia ni Mh. Adam Kimbisa, Mh. Shy Rose Banjhi na Mh. Abdallah Mwinyi wakizungumza na Spika wa Bunge.
J3
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Job Ndugai kulia akizungumza na wabunge hao.
J5
Mkurugenzi wa Mhusiano ya Kimataifa ofisi ya Bunge Bw. Josey Mwakasyuka akijitambulisha katika mkutano huo.
J7
Mh. Shy Rose Banjhi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai kushoto ni Afisa habari wa Bunge Bw. Owen Mwandumbya.

MKE WA RAIS MSTAHAFU NA MWENYEKITI WA WAMAMA ASISITIZA UMUHIMU WA CHAMA CHA GIRL GUIDE TANZANIA KUONGEA WANACHAMA


WAMA1
Mke wa Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa WAMA akisalimiana na Mama Othman Chande alipowasili katika Shule ya Sekondari Tambaza kuhudhuriaWorld Thinking Day iliyoandaliwa na Tanzania Girl Guide Association.
WAMA2
Wanachama wa Girl Guide wakiwasili katika Shule ya Sekondari Tambaza  katika kusherekea World Thinking Day  ambao walipokelewa na Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete.
WAMA3
Mama Salma Kikwete akiingia katika ukumbi wa Tambaza Sekondari akiwa na viongozi wa Girl Guide kushoto ni Mama Symphorosa Hangi, Kamishna Mkuu  na kulia ni Mama Matilda Balama na Mkuu wa Shule ya Tambaza.
WAMA4
Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi  na baadhi ya wanafunzi Wanachama na viongozi wa  Girl Guide
WAMA5
Mama Salma Kikwete akiangalia kazi za wakinamama wajasiriamali ambao walifanya maonyesho katika sherehe hizo

bweni la wavulana shule ya sekondari iyunga jijini mbeya lateketea kwa moto


Moto ukiendelea kuteketeza Bweni la Wavulana (Mkwawa ) katika shule ya sekondari ya
Iyunga jijini Mbeya ambapo chanzo chake kimetajwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo moto huo ulizuka majira ya saa 3 asubuhi february 29 mwaka huu wakati wanafunzi wakiwa madarasani.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa mwenye suti akisaidiana na kikosi cha Zima moto kuuzima moto ulioteketeza Bweni la wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya linalolaza wanafunzi 95 February 29 mwaka huu ambapo hakuna  
 
Muonekano wa bweni la Wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara baada ya kuteketea kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme majira saa3 asubuhi ambapo hakuna mwanafunzi yeyote aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo ya moto. .
 
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa akizungumza na Walimu pamoja na wanafunzi (hawapo pichani )katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara ya baada ya kukumbwa na tukio la kuungua kwa moto kwa mabweni ya wavulana ya (Mkwawa) February 29 mwaka huu.
Kamati ya ulinzi na Usalama wilaya ya  Mbeya na baadhi ya viongozi wakitizama athari zilizotokea mara baada ya mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya kuungua moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme February 29 mwaka huu .
Afisa elimu Mkoa wa Mbeya Charles Mwakalila akizungumzia athari zilizojitokeza mara baada ya mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambayo yaliteketea kutokana na hitilafu ya umeme majira ya saa3 asubuhi wakati wanafunzi wakiwa madarasani .
 
Baadhi ya wanafunzi waliofanikiwa kuokoa vifaa vyao kwa masaada wa watu wa zima moto wakiwa nje wakisubiri utaratibu mara baada ya bweni lao kuteketea kwa moto.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa  nje kusbiri utaratibu mara baada  waliofanikiwa kuokoa baada ya bweni lao kutektea kwa moto.

Sunday, February 28, 2016

WAZIRI NAPE AZINDUA NA KUSHIRIKI KILIMANJARO MARATHON 2016


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na wakazi wa mji wa Moshi waliojitokeza kwa wingi kushiriki mbio za Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo mwaka huu zaidi ya watu elfu 8 walishiriki kutoka nchi mbali mbali ambapo kati ya hao 200 walitoka nchini Kenya. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akikimbia kwenye riadha ya Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo alikimbia kilomita 5 pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Anthony Mtaka, mashindano hayo ya riadha yameshirikisha zaidi ya nchi 40.
 Mshindi wa kwanza wa kilometa 42.2 Kiprotich Kirui akiinua mikono juu kama ishara ya kushangilia ushindi wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2016.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisoma risala mara baada ya kuhitimisha mbio za Kilimanjaro Marathon ambapo aliwapongeza wahiriki wote, wadhamini na kuwataka Watanzania kutumia mbio hizo kama fursa ya kuutangaza utalii uliopo nchini.

MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI MKOANI TANGA KUANZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI MKOANI HUMO LEO


LU1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantum Mahiza alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku Mbili Mkoani humo leo Februari 28, 2016
LU2
Chipukizi wa Umoija wa Vijana wa CCM Mkoa Tanga akimvisha Skafu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani hum oleo Februari 28,2016.
LU3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Vijana wa Chipkizi wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Tanga alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani humo leo Februari 28,2016.
LU4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Tanga baada ya kupokea Taarifa ya Mkoa huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza leo Februari 28, 2016. Makamu wa Rais yupo Mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.
LU5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza leo Februari 28, 2016. Makamu wa Rais yupo Mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.(Picha na OMR)