mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Tuesday, March 1, 2016

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA RAIS MSTAHAFU KIKWETE



halRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia kifo cha Kaka yake Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kilichotokea leo asubuhi nchini India.
Mzee Selemani Mrisho Kikwete alikuwa nchini India kwa matibabu.
Katika salamu zake Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshituko taarifa za kifo cha Mzee Selemani Mrisho Kikwete na amesema anaungana na familia ya Rais Mstaafu Kikwete kuombeleza kifo cha mtu muhimu kwa familia hiyo.
“Napenda kukupa pole nyingi wewe Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, familia yenu yote, ndugu jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mtu muhimu katika familia, natambua uchungu mkubwa mlionao lakini nawaomba muwe  uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu” Alisema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli amemuombea Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete apumzishwe mahali pema peponi, Amina.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Arusha
01 Machi, 2016

No comments:

Post a Comment