WANANCHI wa jamii ya wafugaji wa kimasai wanaoishi katika kijiji cha Chamakweza kata ya Pera Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani wameugomea mpango wa serikali kutaka kukiingiza kijiji hicho katika mpango miji kwani hapo awali eneo hilo walitengewa maalumu kwa ajili ya matumizi ya shughuli za ufugaji tangu mwaka mwaka 1976.
Wafugaji hao wametoa kilio chao kwa waandishi wa habari mara baada ya mkutano wao wa kijiji kuvunjika kutokana na kutokuwa na kibali ambao uliandaliwa kwa ajili ya kuweza kujadili changamoto mbali mbali zinazowakabili ikiwemo uvamizi wa eneo lao pamoja na serikali kuamua kuwabadilishiwa matumizi katika kijiji hicho bila ya kuwashirikisha.
Wakizungumza kwa uchungu kwa nyakati tofauti kijijini hapo baadhi ya wafugaji akiwemo Rehema Rahimu,Wilison Oledongo,Zakharia Samwel ..wamesema kwamba wanashangaa kuona eneo hilo ililotengwa kwa ajili ya ufugaji linataka kuchukuliwa kwa ajili ya kubadilishiwa matumizi mengine wakati wao wanalitumia kwa ajili ya mifuo pekee na wala hawaitaji huduma ya mipango miji.
No comments:
Post a Comment