mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Tuesday, April 26, 2016

Tanzia: Mke wa Rais Mstaafu wa Kenya Mama Lucy Kibaki Afariki Dunia



Mke wa Rais mstaafu  wa    Kenya, mama Lucy Kibaki amefariki dunia . Lucy alifariki katika hospitali ya Bupa Cromwell mjini London alikokuwa amelazwa.

Alisafrishwa hadi mjini Landon wiki moja iliopita kwa matibabu.

Akithibitisha kifo chake rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa kenya imesikitishwa na kifo cha mama Lucy mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki.

Katika taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari Uhuru amesema bi Lucy amekuwa mgonjwa kwa kipindi cha mwezi mmoja .

Amesema kuwa Kenya imempoteza mwanamke aliyechangia mengi katika maendeleo ya taifa la Kenya hususan katika vita dhidi ya ugonjwa wa ukimwi.

Rais ametuma risala za rambi rambi kwa mtangulizi wake Mwai Kibaki pamoja na familia yake.

Chanzo:BBC

Askofu Dr Malasusa wa (KKK) Akamatwa Ugoni



MUME wa mwanamke anayedaiwa kumkamata ugoni Askofu Dk Alex Malasusa wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania (KKK) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, (DMP) anatafuta watoto waliotoroshwa kwa maelekezo ya Malasusa na Jeshi la Polisi, anandika Josephat Isango.

Akizungumza baada ya kuachiwa huru kutoka polisi kwa tuhuma za kushambulia, amesema watoto wake walichukuliwa na raia mmoja mjerumani aliyeolewa na mtanzania, anaitwa Caroline Shedafa.

Caroline Shedafa ametuhumiwa kuwa ametumia mwanya wa malalamiko ya Mwakilima na Malasusa kwa sababu ya urafiki alifanikiwa kuwatorosha watoto hao na kwamba ana mpango wa kuwasafirisha kwenda nje ya nchi wakati wowote.

MwanaHALISI limemtafuta Shedafa kwa tuhuma hizo, alipokea simu na baada ya kuambiwa kuwa anaongea na MwanaHALISI alikata simu na kukataa kuongea suala hili na mwandishi.

Malasusa anadaiwa kuwa anadaiwa kushirikiana na mfanyakazi wa hospitali ya Muhimbili anayeitwa Julieti, aliyewaambia ndugu wa mume anayenyang’anywa mke wake na malasusa kuwa atakiona.

“Huyu kaka anajidai mjuaji, hapti kitu, utaratibu uko tayari wa kuwasafirisha watoto kwenda nje ya nchi na hatawaona tena, ataishia kuwasikia tu, mimi ni mtu wa Karibu na Askofu Malasusa ndo nawaambia”. Alinukuliwa dada huyo akiongea kwa ujasiri.

Hadi sasa watoto wanaotafutwa na baba yao ambao Jeshi la Polisi linadaiwa kushirikiana na Malasusa licha ya taarifa zao kufika polisi kituo cha Wazo na kutochukuliwa hatua ni Sijenuni, Sephania, na Simon wote wanadaiwa kuwa watoto wa Venance Mwakilima.

Taarifa za leo usiku zilizofikiwa MwanaHALISI online zinadai kuwa baadhi ya Maaskofu Jijini Dar es Salaam wameamua kujitokea kulinda heshima ya uaskofu baada ya kudhalilishwa na Malasusa.

Maaskofu ambao hawakupenda kutajwa majina yao kwa kuwa si wasemaji wa vikao halali wamesema “hili suala tunalichukua,

Malasusa ana tuhuma nzito nchini, na baada ya gazeti kuandika watu wamejitolea kujieleza tunaomba muda kesho (Jumanne) tutaliongelea hadharani baada ya kukutana na mume wa me.
Aidha Malasusa hakupatikana kwenye simu zake wala kujibu ujumbe wa simu aliotumiwa tangu juzi wakati gazeti la MwanaHALISI likiendelea kufuatilia sakata hili.

Taarifa ambazo mwandishi anazo zinadai viongozi wakubwa wa serikali wanaingilia suala hili, zinafuatiliwa na zitaandikwa kwenye gazeti la MSETO…

Afisa Uchaguzi ahukumiwa kifungo cha Miaka 7 jela kwa Rushwa



Afisa uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Bw.  Julius Bujabhi Makwasa amehukumiwa kifungo cha Miaka 7 jela baada ya kupatikana na hatia ya Makosa 34 yakiwepo ya Rushwa.

Mnamo mwaka 2013 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mara ilimfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Serengeti Afisa uchaguzi wa Halmashauri hiyo Bwana Julius Bujabhi Makwasa na wenzake wawili wakishitakiwa kwa makosa thelathini na manne yakiwemo ya matumizi mabaya ya fedha za umma, kuisababishia hasara Halmashauri ya Serengeti, kusaidia kutenda kosa, kughushi na kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri wao.

Washitakiwa wengine katika shauri hilo la uhujumu Uchumi E.C.C 130/2013 lililokuwa likisikilizwa na Hakimu wa Mahakama hiyo Mheshimiwa Ismail Emanuel Ngaile,  walikuwa  Bi Scola Daudi Mosi ambaye ni mtunza kumbukumbu wa Halmashauri hiyo na Bwana Dickson Julius Makwasa ambaye ni mtoto wa mshitakiwa wa kwanza.

Ilidaiwa na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Wakili Martin Makani mbele ya mheshimiwa Ngaile kwamba mshitakiwa wa kwanza Julius Makwasa  ambaye majukumu yake yalikuwa pamoja na kuviteketeza vifaa vya uchaguzi muda wa uchaguzi unapopita na mshitakiwa wa pili Scola Mossy ambaye  majukumu yake ni pamoja kusimamia kumbukumbu zinazoingia na zinazotoka nje ya Halmashauri hiyo,  kwa nafasi zao hizo,  walikuwa na jukumu la kuharibu nyaraka za uchaguzi mkuu wa Octoba 2010 kama ilivyokuwa imeelekezwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi.

Katika kutekeleza jukumu hilo ilielezwa kwamba, waliandaa majina ya vibarua na kuingiza majina hewa ishirini na tano (25) kuonyesha kwamba majina hayo hewa pia yalishiriki  kuchimba mashimo, kusomba nyaraka hizo za uchaguzi na kuzipeleka kwenye mashimo kisha kuziteketeza kwa moto hivyo kustahili malipo.

Katika udanganyifu huo ilielezwa kwamba, mshitakiwa wa kwanza na wa pili waliweza kuandaa nyaraka za kuipotosha Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na kuwawezesha kujipatia jumla ya shilingi million tatu laki nane na elfu hamsini (Tsh 3,850,000/=) kwa kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri .

Watu Watatu Wakamatwa na Madawa ya Kulevya Aina ya Mirungi Mkoani Kilimanjaro



Watu watatu akiwemo raia wa Kenya wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya Mirungi na Bangi kilo 54 na misokoto ya Bangi 4,500 ikisafirishwa kutoka nchini Kenya kwenda mkoani Arusha.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Bw.Wilbrod Mutafungwa amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika maeneo ya njia panda Himo wilaya ya Moshi na Sanya juu wilaya ya Siha wakiwa wameficha madawa hayo ya kulevya kwenye miili yao kuanzia maeneo ya tumboni hadi miguuni.

Amewataja waliokamatwa ni Vitalis Victor mfanyabiashara mkoani Arusha, Naftal Mvoyi mkazi wa Voi nchini Kenya, Maulid Maulis mkazi wa Arusha ambao walikuwa wakisafirisha Mirungi kilo 44 kwa kutumia magazeti na gundi ya karatasi na kisha kuifunika kwenye nguo walizokuwa wamevaa wakitokea nchini Kenya kuelekea jiji la Arusha.

Ripota wetu amefanikiwa kuzungumza na baadhi ya vijana wanaojihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya katika manispaa ya Moshi na kueleza kwamba changamoto kubwa inayowabaili ni ukosefu wa ajira hali inayowasababisha baadhi yao kujihusisha na matukio ya uhalifu.

Matumizi ya madawa ya kulevya yameathiri vijana wengi kiafya kutokana na baadhi yao kushindwa kufanya shughuli za maendeleo na hivyo kulazimika kujihusisha na matukio ya wizi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji Amemtaka Rais Magufuli Apunguze Utumbuaji Majipu




Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji amemtaka Rais Magufuli apunguze utumbuaji majipu. Adai inadhalilisha Watumishi wa Serikali

Alisema pamoja na kuwa CHADEMA wanaunga mkono kitendo cha kuwashughulikia mafisadi pamoja na watumishi wasio timiza majukumu yao ipasavyo lakini hawako tayari kuendelea kushuhudia ambavyo amekua akivunja sheria za nchi. “Watumishi wengi wamedhalilishwa na serikali hii ambayo imekuwa ikitumia mabavu kuwawajibisha watu bila kufuata sheria za nchi,” alisema Dk, Mashinji. “Suala la rushwa katika nchi ni jambo la kimfumo ambapo kila unapoona kunamtu katumbuliwa kwaajili ya rushwa basi kuna idadi kubwa ya watu ambao wanashiriki katika rushwa hiyo,” aliongeza Dk Mashinji.

Aidha, alisema kuwa utaratibu wa Rais kuwatumbua watumishi kwenye mikutano ya hadhara kwa kutumia ushabiki wa wananchi hauwezi kulisaidia taifa kufanikiwa katika kuwaletea mabadiliko ya kweli wananchi wake. “Magufuli ametumbua watumishi wengi sana tangu aingie madarakani lakini niwaulize sukari imeshuka bei au mchele umeshuka bei lakini kila siku tunasikia watu wametumbuliwa bila kuwa na tija kwa taifa,” alisema.

Aliwataka vijana wa vyuo vikuu nchini kuungana na CHADEMA katika kuhakikisha serikali inaruhusu kuonyeshwa kwa vipindi vya Bunge moja kwa mpja kama ilivyo kuwa hapo awali.

Breaking Newa: Rais Magufuli Aivunja Bodi ya TCRA na Kumsimamisha Kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hiyo Dr Ally Yahaya Simba



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya Simba kutokana na kutosimamia ipasavyo Mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS), na kusababisha nchi kupoteza mapato ya takriban shilingi bilioni 400 kwa mwaka.

Rais Magufuli amechukua hatua hiyo leo tarehe 26 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao cha kazi kati yake na viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya fedha na Mipango na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Tarehe 22 Machi, 2013 Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) iliingia mkataba na kampuni ya SGS juu ya uwekaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya simu ambapo kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano lakini mpaka sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo kinachohusiana na uthibiti wa mapato ya simu za ndani (Offnet), hali ambayo imesababisha serikali kukosa mapato yanayokadiriwa kuwa shilingi bilioni 400 kwa mwaka.

Pamoja na kuivunja bodi ya TCRA inayoongozwa na Profesa Haji Semboja na Kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba, Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa kumteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo mara moja.

Aidha, Rais Magufuli amewataka Waziri Prof. Mbarawa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu katika wizara hiyo kuchukua hatua mara moja ili mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya simu kwa simu za ndani (Offnet) uanze kufanya kazi, na nchi ipate mapato yanayostahili kukusanywa.

“Waziri hakikisha unachukua hatua mara moja, nataka tukusanye mapato yote ya serikali yanayostahili na sitasita kuchukua hatua  dhidi ya yoyote atakayekwamisha jambo hili” Amesisitiza Rais Magufuli.

Gerson Msigwa

Monday, April 25, 2016

Mapishi ya makande ya nazi na karanga

Inawezekana umeshakula sana makande. Lakini haya ni mapishi tofauti kiasi. Katika mapishi haya tunatumia nazi na karanga. Ni chakula bora chenye ladha bora na kukupa hamu ya kujiramba. Kama mumeo huwa hashibi makande, inabidi uongeze kipimo maana utamu wake unaweza kumfanya amalize chakula cha familia nzima.

Mahitaji

  • Mahindi yaliyokobolewa – kilo 1½
  • Maharage ½ kilo
  • Vitunguu maji 3
  • Nyanya 2
  • Karanga ¼ kilo
  • Njugu mawe ½ kilo 
  • Pilipili hoho 1
  • Chumvi kijiko 1 cha chai
  • Mafuta ¼ lita
  • Nazi kubwa 2.

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

  • Chambua maharage, mahindi, karanga nanjugu mawe kisha osha vizuri.
  • Changanya maharage, mahindi na njungumawe pamoja.
  • Bandika sufuria ya maji jikoni. Weka mchanganyiko wa maharage, weka chumvi kisha acha mchanganyiko uchemke vizuri. Kwa kawaida maharage yanachukua muda mrefu kuiva vizuri. Hivyo unaweza kusubiria takribani dakika 25-30 ili kuhakikisha yameiva. Kama maji yakikauka kabla ya maharage kuiva, ongeza maji kiasi ili yaive vizuri.
  • Andaa vitunguu, pilipili hoho na nyanya kwa kuosha kisha kuvikata vipande vidogo vidogo. Weka vizuri na kusubiria kuvichanganya na makande.
  • Andaa tui la nazi kwa kuchuja tui zito ili liwe tayari kuchanganya na chakula.
  • Kama maharage na njugu mawe yakikaribia kuiva (takribani dakika 30) weka karanga kwenye mchanganyiko. Koroga ili vichanganyike vizuri. Acha iendelee kuchemka na subiria hadi mchanganyiko uive vizuri. Mchanganyiko ukiiva vizuri toa jikoni na hifadhi pembeni.
  • Bandika sufuria, weka mafuta ya kula kisha acha yachemke.
  • Mafuta yakipata moto vizuri weka vitunguu kisha koroga koroga hadi vibadilike rangi na kuanza kuwa na rangi ya udongo.
  • Weka pilipili hoho, karoti. Koroga kiasi kwa muda wa dakika 2 hadi 3.
  • Weka nyanya, koroga kiasi na kisha funika na mfuniko. Acha nyanya ziive vizuri kwa mvuke ili ziwe laini. Baada ya dakika 6-8 unaweza kuponda ua kusaga nyanya ili kupata mchuzi wenye rojo. Koroga ili kupata mchanganyiko mzuri.
  • Nyanya zikiiva vizuri weka mchanganyiko wa maharage kwenye sufuria. Koroga vizuri hadi mchangyiko uwe sawia. Onja ili kujua kama kiwango cha chumvi kinatosha. Unaweza kuongeza kama haitoshi.
  • Weka tui la nazi huku ukikoroga ili kuzuia tui kukatika. Koroga hadi ianze kuchemka.
  • Funika sufuria na subiria kwa muda wa dakika 10, kisha ipua chakula jikoni ili upate kujiramba.

CAG Kuanika Mafisadi Bungeni Leo Wakati Akiwasilisha Ripoti Yake



Mdhibiti  na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) leo anawasilisha bungeni ripoti ya mwisho ya ukaguzi wa hesabu za serikali ya mwaka 2014/15.

Ingawa haijajulikana rasmi nini kilichomo ndani yake, baadhi ya watu waliohojiwa wanatarajia CAG kubaini mchwa wanaotafuna fedha za umma na namna ya kukabiliana nao.

Aidha wengine wanatarajia taarifa ya hali bora zaidi ya usimamizi wa fedha za umma kuliko kipindi cha nyuma.

Ripoti hiyo awali ilikuwa imepangwa kuwasilishwa bungeni mwishoni mwa wiki (Aprili 22) kabla ya kuahirishwa hadi leo.

“Ni kweli CAG atawasilisha ripoti kesho (leo) bungeni, ”Naibu Katibu wa Bunge na Utawala, Joel Joel alithibitisha juu ya kuwasilishwa kwa ripoti hiyo leo. 

Miongoni mwa wabunge waliozungumza na mwandishi wa habari hizi, wamesema wanatarajia CAG kuonesha mambo mazuri kwa maana ya taasisi zilizofanya vizuri katika usimamizi wa fedha za umma lakini pia mambo mabaya.

“Lazima ripoti itaibua madudu maana walizoea (watendaji serikali) kana kwamba hapakuwapo na serikali,” alisema Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy na kusisitiza kuwa pamoja na wabunge wenzake, watamsaidia Rais John Magufuli kupambana na ubadhirifu serikalini.

Keisy alisema akiwa mbunge, anaamini pamoja na wenzake, wanachosubiri ni kuona ripoti hiyo na kuhakikisha wanaohusika na kuchezea fedha za serikali, kabla ya kufikishwa mahakamani, wanarudisha fedha hizo.

“Atakachosema CAG sisi tutakuwa tayari kusimama kusaidia Rais aendelee kupambana na ubadhirifu,” alisema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mbinga Vijijini, Martin Msuha, alisema ripoti hiyo ni muhimu katika usimamizi wa serikali na inategemewa kuwa na mambo mazuri na mabaya kwa maana ya majipu ambayo yatapaswa kutumbuliwa.

Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jasson Rweikiza alisema matarajio waliyo nayo ni kwamba ubadhirifu na wizi utakaoibuliwa na ripoti hiyo utashughulikiwa mara moja.

 “Kama kuna ubadhirifu, mishahara hewa na wizi vyote vishughulikiwe...kama kuna ubadhirifu na wizi wowote, mwizi mahali pake ni jela,” alisema Rweikiza akishutumu uwapo wafanyakazi hewa katika halmashauri yake.

Paul Okoye wa kundi la P-Square Anaswa South Africa Akiwa Amevaa Kofia ya WCB Wasafi ya Diamond..



Ukimuona Paul Okoye wa kundi la P-Square akiwa amevaa kofia ya WCB na yupo Johannesburg, Afrika Kusini ambako Diamond yupo huko tangu mwanzoni mwa wiki hii kuzindua video ya Colors of Africa, ujue mambo yameiva.

Paul amepost picha Instagram akiwa amevaa kofia nyeupe ya WCB, label ya Diamond na kuashiria kuwa huenda wiki hii wakali hao wakashoot video ya collabo yao. Diamond aliingia studio na P-Square mwaka jana.

Kituo cha runinga cha MTV Base kiliripoti wiki hii kuwa Diamond atashoot video ya wimbo huo hivi karibuni.

Habari Mbaya Kutoka Ubelgiji...Mchezaji Samatta Aumia Pua Mchezoni..Anasubiri Vipimo Kujua Kama Pua Imevunjika



Jumapili April 24 usiku timu ya Genk ilishuka dimbani kuchuana na Gent lakini taarifa mbaya kuhusu star wa Bongo kwenye ligi ya Ubelgiji Mbwana Samatta ni kwamba, amepata majeraha katika mchezo huo ambao alianza kwenye kikosi cha kwanza lakini hakuweza kumaliza dakika zote 90.

Kipindi cha pili Samatta alishindwa kurudi uwanjani kuendelea na mchezo kutokana na maumivu aliyoyapata kipindi cha kwanza baada ya kugongwa pua. Ilibidi nafasi yake ichukuliwe na Nikolaos Karelis aliyeingia dakika ya 46 kipindi cha pili.

Timu ya Genk imepoteza mchezo wake wa Jupiter League baada ya kukubali kipigo cha 2-1 vs Gent.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 25, Ikiwemo Takururu Kuchunguza Mabilioni ya Kikwete




SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 25, Ikiwemo Takururu Kuchunguza Mabilioni ya Kikwete

Mwafrika wa Kwanza Kushinda Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kulipwa Ulaya Ametangazwa, Amewahi Kuifunga Tanzania



Usiku wa April 24 imetangazwa good news  kwa soka la Afrika, huu sio ushindi wa taifa la mchezaji husika ila  ni fahari ya Afrika nzima, winga mshambuliaji wa kimataifa wa Algeria anayeichezea klabu ya Leicester City ya Uingereza Riyad Mahrez ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya PFA 2015/2016 (Professional Footballers Association).

Riyad Mahrez ametangazwa kushinda tuzo hiyo mbele ya wachezaji kama Mesut Ozil wa Arsenal, Jamie Vardy wa Leicester City, Harry Kane wa Spurs, N’golo Kante wa Leicester City, Dimitri Payet wa West Ham United, PFA ni tuzo za wachezaji bora wa kulipwa.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Riyad Mahrez ndio alikuwa mchezaji wa Algeria aliyefunga goli la nne dakika ya 43 katika ushindi wa goli 7-0 dhidi ya Taifa Stars November 17 2015 na kuIondoa Tanzania katika mbio za kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2018.

Vyeti Feki Vitampa Magufuli Maadui Wengi kuliko Hata "Ufisadi"



Kama kweli Rais Magufuli atahamia katika ukaguzi wa vyeti feki akimaliza ishu ya watumishi hewa ni wazi atapata maadui wengi na idadi yao itakuwa kubwa kuliko anaowapata katika vita yake dhidi ya ubadhirifu.

Watumishi wenye vyeti feki katika utumishi wa umma na makampuni binafsi ni wengi mno. Wengi wao wanafahamika na ndugu zao, marafiki zo na hata majirani zao kwa aidha kufahamu historia zao au kwa kutumia majina tofauti na yale waliyozaliwa nayo au kubatizwa nayo.

Wengi wa watumishi hawa wamepanda ngazi mbalimbali katika utumishi wa umma na hata wengine kufikia ngazi za juu. Wakati mchakato wa vitambulisho vya taifa ulipoanza suala hili linasemekana lilijitokeza kwa kiasi kikubwa katika idara nyeti za serikali lakini kutokana na ukubwa wake ikaamuliwa lifumbiwe macho.

Vyeti feki vinagusa karibu kada zote na katika ngazi mbalimbali mpaka hata zile ngazi zinazoonekana za watu wasioguswa.

Kama Rais JPM akiingia nakugusa huku ni wazi atakuta amegusaa idadi kubwa ya watanzania ikiwemo ile inayomuunga mkono. Tegemezi wa vyeti feki na vyeti feki wenyewe wataendelea kumuunga mkono zamu yao ya kutumbuliwa ikifika? Ndio maana nachele kusema kuwa zoezi la utambuzi wa vyeti feki litamuacha Rais Magufuli na maadui wengi kuliko atakaowapata katika zoezi la ubadhirifu hivyo serikali yake inaweza kupoteza umaarufu ilioanza kuupata. Homa imepanda kiasi kwamba wenye vyeti feki wanaongoza mashambulizi makali ya ukosoaji katika mitandao ya kijamii na popote wapatapo fursa dhidi ya utendaji wa JPM ili kumpunguza nguvu.

Kauli ya Kwanza ya Mkurugenzi wa TFF Baada ya Mchezo wa Yanga na Coastal Union Kuvunjika Jana...



Baada ya mchezo huo kuvunjika uliyokuwa unarushwa Live kupitia Azam Tv, ripota wa Azam Tv alifanya mahojiano mafupi ya Live kutoka katika uwanja wa Mkwakwani Tanga na kaimu mkurugenzi wa mashindano wa TFF Jemedali Said ilikujua mambo yatakuwaje mchezo utarudiwa au inakuwaje?

“Kiukweli mchezo umevunjika lakini haya mashindano yanaendeshwa kwa kanuni na taratibu ila sisi tunasubiri ripoti ya muamuzi na kamisaa wa mchezo ili tuweze kufanya maamuzi” Alisema Jemedali Sai

Saturday, April 23, 2016

Sheikh Mkuu Akerwa Tabia za Akina Wema Sepetu


Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim amesema anakerwa na mastaa wanaodaiwa kuwa na tabia chafu zenye viashiria vya usagaji.

Shehe huyo aliyasema hayo hivi karibuni baada ya kutafutwa na gazeti hili kufuatia kusambaa kwa picha mitandaoni zinazomuonesha mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’ akiwa kwenye pozi la kimahaba na mwanamuziki Diana Exavery ‘Malaika’.


“Vitendo hivyo vinavyoashiria tabia za usagaji ni machukizo kwa Mwenyezi Mungu, pia ni laana na havikubaliki kabisa katika imani yeyote, anayefanya vitendo hivyo anatakiwa kuachana navyo maana havimpendezi Mungu.

“Wasanii wote, wanapaswa kutambua kuwa wao ni kioo cha jamii na watu wanahitaji kujifunza mambo mengi mazuri kutoka kwao na si kuwapotosha,” alisema Shehe Alhadi.


Ikumbukwe kuwa hii si mara ya kwanza kwa Wema Sepetu kujianika akiwa kwenye mapozi ya kimahaba na wanawake wenzake, alishawahi pia kuonekana katika pozi tata na mwigizaji Aunt Ezekiel.

Juma Abdul Jaffar Mnyamani Awa Lulu Yanga...Wamsainisha Mkataba Mpya Fasta


BEKI hodari wa kulia wa kimataifa wa Tanzania, Juma Abdul Jaffar Mnyamani amesaini Mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga SC ya Dar es Salaam hadi mwaka 2018.

Habari kutoka ndani ya Yanga zinasema kwamba Abdul alisaini Mkataba huo kabla ya timu hiyo kwenda Misri kucheza na Ahly.

Na hakuna kingine kilichoisukuma Yanga kumsainisha Mkataba mpya beki wake huyo zaidi ya kiwango chake kizuri kwa sasa akionekana kabisa kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu kikosini.

Na kwa kusaini Mkataba huo, Juma ataingia kwenye orodha ya wachezaji walioitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu.

Juma aliyezaliwa Novemba 10, mwaka 1992
Mwananyamala, Dar es Salaam, alijiunga na Yanga mwaka 2012 akitokea Mtibwa Sugar kwa Mkataba wa miaka miwili, ambao ulipoisha akaongezwa mwingine wa miaka miwili.

Na wakati Mkataba wake wa sasa unaelekea kumalizika mwishoni mwa msimu, inaelezwa tayari Juma Abdul amesaini Mkataba mwingine mpya wa miaka miwili utakaomfanya afikishe miaka sita Jangwani.

Matokeo ya Mechi Kati ya Chelsea na Bournemouth Haya Hapa...


Kiungo wa Chelsea, Willian akimvisha kanzu kipa wa Bournemouth, Boruc kumalizia pasi ya Fabregas kuifungia Chelsea katika ushindi wa 4-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Vitality. Mabao ya Chelsea yamefungwa na Pedro, Hazard mawili na Willian, huku la wenyeji likifungwa na Elphick Uwanja wa

Kosa la Kutukana Kwa Kutumia Mtandao ndio Chanzo cha Siwema wa Nay wa Mitego Kutupwa Jela Miaka Miwili


Mahakama kuu ya mkoani Mwanza imemuhukumu Siwema ambaye ni mzazi mwenzake na Nay Wamitego miaka miwili jela kwa kesi ya kumtukana mtu kwa njia ya mtandao.

Siwema alituhumiwa kumtukana matusi kwa njia ya mtandao mlalamikaji ambaye anafahamika kwa jina la Deo.

Akizunguza na kipindi cha Jahazi, kinachoruka kupitia Clouds FM, Nay Wamitego alisema ‘napambana kile nitakachoweza kuangalia kama kunauwezekano wa kumpa msaada’.

“Kuna vitu nafikiria kuvifanya ili kujaribu kumsaidia, baada ya kupata hizi taarifa kidogo kama siko sawa hivi. Ni mzazi mwenzangu mimi nay eye tulikaa muda mrefu, napambana kile nitakachoweza kuangalia kama kunauwezekano wa kumpa msaada mwingine kwa njia yeyote ili asiwe kwenye mazingira ambayo tayari ameshawekwa. Anayemshtaki najua anaitwa Deo, jina jingine silifaham,” aliongezea.

Nay na Siwema walifanikiwa kukaa kwenye mahusiano kwa kipindi kirefu na kufanikiwa kupata motto mmoja, Curtis kabla hawajachana na kila mtu kushika njia yake.

Friday, April 22, 2016

HAKUNA MAREFU YASIYO NA NCHA HATIMAYE SEMINA YA UJASIRIAMALI YAFIKA TAMATI KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA















Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Massawe maarufu kwa jina la Kompyuta wizadi akifundisha njia mbalimbali za kutunza kumbukumbu za mapato ya biashara



Bw Massawe ameelezea njia tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na kuwa na kitabu mbalimbali vya mapato ambavyo humsaidia mjasiriamali katika kufanya mahesabu ya biashara yake
























Wanafunzi wakifanya biashara katika ukumbi wa chuo hicho  baada ya kupata semina ya ujasiriamali




Makamo mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Ausha akifunga semina hii ya ujasiriamali iliyoanza tangu siku ya Jumatatu na kufikia kikomo siku ya leo



Kwa niaba ya mkurugenzi wa mafunzo katika chuo hicho Bw Elifuraha Samboto  ambaye ni makamo mkuu wa chuo ametangaza rasmi kufungwa kwa semina hiyo


Amewahasa wanafunzi kutokujiwekea dhana ya kutokuajiriwa pindi wamalizapo chuo kwani baadhi yao baada ya kupata semina hiyo wamekata tamaa ya kutokuajiriwa na kujiajiri wenywe

"Wengi wao wamesema hawataajiriwa na mtu yeyote pindi wamalizapo chuo, hilo wazo ni zuri ila lazima uwe na mtaji wa kujiajiri ,nawshauri  wanafunzi waajiriwe ili waweze pata mtaji pia kupata uzoefu wa mambo mbalimbali ya kibiashara"Alisema Bw. Samboto

semina ya ujasiriamali yafika tamati katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha ndani ya mwaka huu wa 2016















Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Massawe maarufu kwa jina la Kompyuta wizadi akifundisha njia mbalimbali za kutunza kumbukumbu za mapato ya biashara



Bw Massawe ameelezea njia tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na kuwa na kitabu mbalimbali vya mapato ambavyo humsaidia mjasiriamali katika kufanya mahesabu ya biashara yake
























Wanafunzi wakifanya biashara katika ukumbi wa chuo hicho  baada ya kupata semina ya ujasiriamali




Makamo mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Ausha akifunga semina hii ya ujasiriamali iliyoanza tangu siku ya Jumatatu na kufikia kikomo siku ya leo



Kwa niaba ya mkurugenzi wa mafunzo katika chuo hicho Bw Elifuraha Samboto  ambaye ni makamo mkuu wa chuo ametangaza rasmi kufungwa kwa semina hiyo


Amewahasa wanafunzi kutokujiwekea dhana ya kutokuajiriwa pindi wamalizapo chuo kwani baadhi yao baada ya kupata semina hiyo wamekata tamaa ya kutokuajiriwa na kujiajiri wenywe

"Wengi wao wamesema hawataajiriwa na mtu yeyote pindi wamalizapo chuo, hilo wazo ni zuri ila lazima uwe na mtaji wa kujiajiri ,nawshauri  wanafunzi waajiriwe ili waweze pata mtaji pia kupata uzoefu wa mambo mbalimbali ya kibiashara"Alisema Bw. Samboto