WAKALA wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) unahitaji kiasi cha Sh milioni 300 ili kukamilisha baadhi ya matengenezo yanayohitajika kufanyika kwa haraka katika vituo vya mabasi kabla kuanza utoaji huduma ambao serikali imesema utaanza rasmi mwezi ujao.
Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Kaimu Meneja wa Miundombinu wa Dart, John Shauri alisema fedha hizo ni kati ya Sh bilioni 3.2 ambazo zinahitajika kukamilisha sehemu ya kwanza ya Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (BRT).
“Ili mradi huu uanze kufanya kazi tunahitaji kwa haraka kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya kukamilisha kazi zilizosalia ikiwa ni pamoja na ujenzi wa uzio, kuajiri watumishi na kufanya kampeni mbalimbali za kuelimisha umma juu ya mradi huo,” alisema Shauri.
No comments:
Post a Comment