mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Monday, April 4, 2016

WAZIRI KITWANGA APIGA MARUFUKU KUCHEZA “POOL TABLE” WAKATI WA KAZI JIMBONI KWAKE


POO1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia) akizungumza na wananchi wa mji wa Misungwi kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya jimbo hilo. Katika hotuba yake, Kitwanga aliwaka wananchi hao kufanyakazi ili jimbo hilo lizidi kusonga mbele. Pia Mbunge huyo alipiga marufuku uchezaji wa pool table wakati wa kazi. 
POO2
Mkazi wa Misungwi mjini, Songoro Msafiri (kushoto) akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia aliyekaa), mara baada ya Mbunge huyo kumaliza kuzungumza na wananchi hao na kuruhusu kuuliuzwa maswali mbalimbali yanayowakera jimboni humo. Kitwanga aliwataka wananchi wa jimbo lake washirikiane ili waliletee maendeleo jimbo lao.
POO3
Wananchi wa mjini Misungwi wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini huo leo.
POO4
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na mabalozi wa mashina wa CCM katika Ukumbi wa Mikutano wa CCM Wilaya ya Misungwi. Kitwanga aliwashukuru mabalozi hao kwa kumchagua na kuwaomba washirikiane zaidi ili kuliletea maendeleo jimbo hilo. Picha zote na Felix Mwagara

No comments:

Post a Comment