mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Wednesday, March 2, 2016

MAKAMU WA RAIS BI. SAMIA SULUHU HASSAN MGENI RASMI TAMASHA LA WANAWAKE


tm1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Bi. Agnes Mgongo (katikati) akiongea na waandishi wa  habari kuhusu   tamasha  la pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016, ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Bi. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kushoto kwake ni Mratibu wa tamasha hilo Bi. Anawery Phares na kulia  ni  mshehereshaji (MC Pilipili) Bw. Emanuel Mathias.
Mratibu wa Tamasha la pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016 Bi. Anawery Phares(katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu tamasha hilo ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe. Bi. Samia Suluhu Hassan,Kushoto ni Mwanamuzi wa Taarabu Bi. Patricia Hillary na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark  Bi.Agnes Mgongo.
tm3
Mchekeshaji na Mshehereshaji  Bw. Emanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili akito kionjo cha mojawapo ya kichekesho atakachokifanya siku ya tamasha la pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016,kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark  Agnes Mgongo na kulia ni Mwakilishi wa Children Survial Hut Tanzania (CSI) Bi.Stella Mranda.
tm4
Msanii wa Muziki wa Taarabu Nchini Bi .Patricia Hillary akieleza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu  kwa tamasha la pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016 ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Bi. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.(Picha na Lorietha Laurence-Maelezo).
…………………………………………………………………………………………………………………..
Na Beatrice Lyimo-Maelezo
Dar es Salaam,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia litakalofanyika Machi 5, 2016.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam  na Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark  Agnes Mgongo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya tamasha hilo ambalo litafanyika katika ukumbi wa King Solomoni uliopo Nanga jijini Dar es salaam kwa kujumuisha jinsia zote .
Ameongeza kuwa Kampuni ya Trumark imeandaa tamasha hilo kwa lengo la kuwahamasisha wanawake kuwa na nguvu katika nafasi ya kuchangia na kuinua uchumi na maendeleo ya nchini.
“Ni kweli wapo wanawake wenye mafanikio lakini  kuna changamoto zinawakabili  ikiwemo uchache wa ushiriki wa wanaume katika kufanikisha mafanikio ya wanawake na kufungua fursa ili waweze kuwa sehemu ya mafanikio kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii” alifafanua Agnes.
Mbali na hayo Bi. Agnes amesema kuwa kila mtu kwa nafasi yake ni kiongozi wa kuleta chachu ya maendeleo, hivyo kila mtu na mahali popote alipo ashiriki vyema kutimiza wajibu wake huku wakishirikiana na kusaidiana kwa pamoja ili kujenga taifa.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na masuala ya watoto na wanawake  (CSI Tanzania) nchini Stelala Mranda amesema kuwa  wameahidi kuwawezesha wanawake 20 watakaotaka kuhudhuria tamasha hilo.
Wadau mbalimbali wakiwemo Marie stopes Tanzania, CSI Tanzania, wamejitokeza kudhamini tamasha hilo lililobeba kauli mbiu isemayo “Pamoja tutafanikisha”.
Tamasha hilo linatarajiwa kuanza saa saba mchana kwa huduma za bure za upimaji na ushauri wa njia za uzazi wa mpango, upimaji wa saratani  ya mlango wa uzazi kwa washiriki na wananchi wote watakao hudhuria tamasha hilo.
Tamasha hilo linatarajiwa kuanza saa saba mchana kwa huduma za bure za upimaji na ushauri wa njia za uzazi wa mpango, upimaji wa saratani  ya mlango wa uzazi kwa washiriki na wananchi wote watakao hudhuria tamasha hilo.

No comments:

Post a Comment