MBUNGE wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Mh. Venance Mwamoto amesema kuwa lengo la wananchi wa Kilolo kumchagua kuwa mbunge wao ni kutaka kuona analeta maendeleo jimboni na sio kuwavunjia heshima wapiga kura wake kwa kuwa mbunge bingwa wa kusinzia bungeni ama kushiriki vurugu zisizo na tija silengo la wana Kilolo .
Akizungumza leo katika mkutano wake wa hadhara katika kata ya Ng’ang’ange mkutano wa kuwashukuru wananchi wa Kilolo kwa kumchangua kuwa mbunge wao kwa ajili ya kutaka kuona wilaya hiyo ya kilolo inapiga hatua katika maendeleo na si vinginevyo .
Hivyo alisema kuwa mbali ya kuwa wapo baadhi ya watu wachache hasa wapinzani wake katika siasa ambao wanazunguka maeneo mbali mbali ya jimbo hilo na kumchafua kuwa amefungiwa kwa muda wa miezi sita kushiriki vikao vya bunge kwa madai ya kuuliza swali la kupigania maendeleo ya Kilolo ,alitaka wananchi wa Kilolo kupuuza maneno hayo kwani hakuna jambo kama hilo na yeye hajapata kufungiwa wala kuonyo bungeni .
“Naomba mtambue huu si wakati wa kampeni ni wakati wa mimi kama mbunge wenu kwa kushirikiana na rais Dr John Magufuli na madiwani kuona kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi inafanyika ila wapo wapinzani wachache ambao wanazunguka katika minada na kueleza uzushi usio na kichwa wa miguu kuwa eti mbunge wa Kilolo amefungiwa na Rais Dr Magufuli kushiriki vikao vya bunge kwa madai kuwa kwanini nataka kujenga chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali teule ya wilaya ya Kilolo iliyopo Ilula” Mbunge Mwamoto alisema maneno hayo yasiwakatishe nguvu wananchi wa Kilolo kweani hakuna kitu kama hicho na Rais hausiki na kumwajibisha mbunge wala diwani pia hata sipika hajapata kumnyoshea kidole wala kumpa onyo lolote na kuwa siku zote mti unaopigwa mawe ndio wenye matunda na yeye atazidi kuwaletea maendeleo wananchi wake kama alivyoanza na kuwataka wapinzani na wana CCM kuachana na siasa za majukwaani kwa sasa ni muda wa kazi.
Hata hivyo mbunge Mwamoto alisema kuwa lengo lake ni kufanya kazi kwa moyo wote ili kuifanya wilaya ya kilolo isonge mbele zaidi kimaendeleo na katika kuonyesha kwa vitendo kuwa yeye si mbunge wa kulala ni mbunge wa kazi ataomba diwani wa kata hiyo kuandaa ukumbi wa kijiji ili alete Runinga kwa ajili ya wananchi wakitoka shamba kufuatilia vikao vya bunge ili kuona kama ni mbunge wa kusinzia bungeni ama kazi.
Alisema iwapo wananchi wake watabahatika kuona anasinzia bungeni pindi atakaporejea kutoka bungeni wasisite kumuuliza sababu ya yeye kusinzia bungeni.
|
Thursday, March 3, 2016
MBUNGE WA KILOLO MH. VENANCE MWAMOTO AWASHUKURU WANANCHI KWA KUMCHAGUA, AAHIDI KUWATUMIKIA NA SI KULETA VURUGU BUNGENI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment