Wadau nchini wameshauriwa kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwasaidia wazee na watu wasio jiweza katika kutatua changamoto zinazolikabili kundi hilo.
Akizungumza katika hafla ya utoaji wa msaada wa Vyakula, mashine za kifulia, solar panel katika kituo cha kulea wazee na watu wasio jiweza kilichopo Buk
umbi Mkoani Mwanza Mke wa rais Mama Janeth Magufuli alisema kuwa mashirika, taasisi za serikali, makampuni binafsi yanapaswa kuona umuhimu wa kulisaidia kundi hili muhimu linaloelezwa kuwa kwenye mahitaji na uangalizi wa karibu.
umbi Mkoani Mwanza Mke wa rais Mama Janeth Magufuli alisema kuwa mashirika, taasisi za serikali, makampuni binafsi yanapaswa kuona umuhimu wa kulisaidia kundi hili muhimu linaloelezwa kuwa kwenye mahitaji na uangalizi wa karibu.
“Mashirikia, Taasisi za serikali, Makampuni binafsi hamna budi kushirikiana na serikali katika kuhakikisha tunaondoa kabisa changamoto zinazokabili kundi hili, misaada mtakayokuwa mnatoa itasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto hizi kwa kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano iliyojielekeza kuondoa makali ya maisha hasa kwa kundi hili muhimu.
Aidha Mama Janeth alisema kuwa katika nafasi yake atajitahidi kuendelea kushirikiana na Wadau mbalimbali ili kuondoa changamoto kwa Wazee na watu wasiojiweza kote nchini na kuifanya jamii hiyo kuishi katika mazingira salama.
Pia Mama Janeth aliwapongeza wadau wakiwamo Benki ya CRDB, PPF, na kampuni nyingine binafsi kwa misaada waliyoitoa kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza kilochopo bukumbi mkoani mwanza kwani misaada hiyo itasaidia katika kutatua changamoto zilizopo kituoni hapo.
Baadhi ya vitu vilivyotolewa ni Mchele tani 6, Unga tani 6, Maharage tani 3, Mafuta tani 1000, solar panel 11 na mashine ya kufulia.
Katika kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani Mama janeth Magufuli amewataka wanawake kote nchini kutumia fursa ya mikopo inayotolewa na Taasisi mbalimbali nchini katika kujiletea maendeleo.
Naye mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo amewahakikishia wazee hao na Watanzania kwa ujumla kuwa serikali ya awamu ya Tano itaendelea kutekeleza ahadi yake ya kulisaidia kundi hili muhimu katika nyanja zote za maisha ikiwemo huduma ya afya ikiwa ni dhamira ya kuondoa kabisa changamoto zilizokuwa zikiwakabili wazee na watu wasiojiweza kote nchini
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei amemshukuru Mama Janeth kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia Wazee na na watu wasio jiweza na kumuahidi kuiangalia Upya sera ya huduma za jamii ili kuhakikisha wanaongeza wigo katika utoaji wa huduma kwa Wazee na watu wasiojiweza Kote nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Wazee wa Kituo hicho Afisa Mfawidhi na mlezi wa kituo hicho Kilicho chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii Bw. michael Bundala ameshukuru kupata msaada uliotolewa na wadau hao na kuwahakikishia kuwa utasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto zilizokuwa zikikikabili kituo hicho hasa umeme na chakula.
Kituo cha Kulea wazee na watu wasiojiweza cha bukumbi mkoani mwanza kilianzishwa mwaka 1974 chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii.
No comments:
Post a Comment