mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Monday, March 7, 2016

WAFANYABIASHARA WA MATUNDA JIJINI ARUSHA WAMEIOMBA SERIKALI KUWATENGEA MAENEO YA KUFANYIA BIASHARA

WAFANYABIASHARA WA MATUNDA JIJINI ARUSHA WAMEIOMBA SERIKALI KUWATENGEA MAENEO YA KUFANYIA BIASHARA


 
Mfanyabiashara Enock Mwika akiwahudumia wateja katika eneo lake la biashara
Baadhi ya wafanyabiashara wa matunda katika soko la kwa morombo jijini Arusha wameiomba serkali kuwatengea maeneo maalumu kwa ajili ya kufanyia biashara hiyo.

Akizungumza na mbotera one blog katika eneo lake la biashara bw. Enock mwika amesema kuwa serikali imekuwa haiwathamini wafanyabiashara wa matunda sokoni hapo kwani wameshindwa kuwatengea maeneo maalumu kwa ajili ya kufanyia biashara hiyo.
Baadhi ya matunda m

Pia bw. Mwika amesema kuwa wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbli za kufukuzwa barabarani na wafanyakazi wa manispaa huku wakati mwingine kupingwa na kunyang’anywa bidhaa zao.

Aliongeza kwa kueleza changamoto nyingine anayokabiliana nayo ni matunda kuharibika kutokana na kutopata wateja kwa muda muafaka.
Matunda aina ya nanasi yakiwa tayari kuuzwa


Aidha ameuomba uongozi wa manispaa kuwaangalia kwa jicho la tatu wafanyabiashara wadogo wadogo wa matunda katika maeneo mbalimbali jijini humo ili kuhakikisha wanawapangia maeneo maalumu kwa ajili ya kufanyia biashara hiyo. 

No comments:

Post a Comment