Wednesday, 9 March 2016
Mwenyekiti wa mtaa wa FFU bwana Anaclet edward
Bi. Regina Makorongo akichochea moto
Mfanyabiashara wa soko la kwa morombo jijini Arusha Zena Shabaan
Wafanyabiashara wa soko la kwa Morombo wamegomea manispaa ya jiji la Arusha kuhamimia katika eneo lililotengwa na serikali na kusema hawako tayari kutokana na miundo mbinu ya soko hilo kuwa mibovu na kuhofia usalama wa mali zao
Hata hivyo amesema kuwa mtu anapokamatwa na manispaa anatakiwa apelekwe mahakamani na siyo mahali pengine na kuiomba serikali hii ya awamu ya tano iwatengenezee mazingira mazuri ya biashara
“Yaani hawa manispaa wanatunyanyasa kwa kweli, sisi kufanya biashara zetu pembezoni mwa barabara ni kutokana na mazingira ya soko ambalo walitupeleka kuwa mibovu na hakuna ulinzi wowote ambao utaweka hali ya usalama tunalipa kodi sasa hizo pesa zetu za kodi wanazipeleka wapi ?” Alisema mmoja wa wafanyabiashara
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa FFU ambako linapatikanaa soko hilo Bw. Anaclet Edward amesema kuwa eneo wanalofanyia biashara kwa sasa ni kinyume cha sheria kwani mwaka jana walipewa barua ya maandishi wahame eneo hilo lakini cha kushangaza hadi sasa wapo wanaendelea na biashara
Sanjari na hayo Bw. Edward ameongeza kwa kusema yeye hawanyanyasi wananchi wake bali anatekeleza jukumu hilo kwa manufaa yao wenyewe
“Mimi nafanya hivyo kwa ajili ya kuwaweka kwenye usalama kwa siyo tu ni amri kutoka manispaa ya jiji letu hili cha msingi wananchi wafuate kanuni na utaratibu unavyotaka”Aliongea
No comments:
Post a Comment