Mhungaji wa kanisa la Timotheo tawi la TAG lililopo kwa morombo jijini arusha Bw. Raimond Matwi.
Wakristo wote nchini wameaswa kutenda matendo yaliyomema maana mwokozi wa ulimwengu yesu kristo amezaliwa kwa ajili yao.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na mchungaji wa kanisa la Timotheo lililo kuwa Arusha mjini mchungaji Raimond amewaasa wakristo wote kumrudia mungu kwa kutenda matendo yaliyo mema.
Sanjari na hayo amewaomba kusherekea kwa amani na utulivu na kumtaka kila mtu ampende jilani yake kama anavyo jipenda mwenyewe na amsaidie mavazi na chakula pale panapo wezekana nakusema huo ndio ukristo.
Mchungaji Raimond amewataka wakristo waache kuwa watumwa wa zambi na kuwataka wahudhurie katika nyumba za ibada ili kufurahia ujio wa bwana wetu yesu kristo
.
Pia mchungaji huyo ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa namna inavyofanya kazi kwa bidii na kuwaombea aendelee kuwapa nguvu za kufanya kazi kwa bidii
.
Vilevile amelishukuru jeshi la polisi kwa kuendelea kuweka ulinzi na usalama katika mkoa wa Arusha hasa katika kipindi hiki cha kwaresma.

No comments:
Post a Comment